WANAHABARI MARA WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZA AFYA
Shomari Binda
MUSOMA
MUUNGANO wa vilabu vya waandishi wa habari nchini UTPC, umenza kutoa
mafunzo maalum kuandika habari za afya kwa waandishi wa habari katika
mikoa yote nchini.
Hatua hiyo
inalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za afya
zilizofanyiwa utafiti wa kina kwa lengo la kuboresha sekta afya na
kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Mkurugenzi wa UTPC Bw
Aboubakar karssan, ameyasema hayo mjini Musoma wakati wa mafunzo ya
kwanza ya siku nne kuanza kutolewa nchini kwa waandishi wa habari mkoani
Mara ikiwa ni sehemu ya utatuzi wa matatizo na kuibua changamoto
zinazokabili utoaji wa huduma ya afya nchini.
Amesema kwa muda
mrefu jamii imekuwa ikikabiliwa na sintofahamu juu ya kujikinga na
maambukizi ya magonjwa hususan Ukimwi kutokana na waandishi nchini
kutoandika habari ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina ambao haotoi
majibu ya namna ya kujikinga na maambukizi mapya.
Kwa sababu
hiyo ametoa wito kwa wanahabari mkoani Mara kutumia vema nafasi ya
mafunzo hayo kwa lengo la kuibua changamoto zinazokabili sekta ya afya
hasa maeneo ya vijijini ili kuwezesha wananchi kutumia mbinu bora za
kujikinga na maradhi.
Kwa mujibu wa mwezeshaji wa mafunzo hayo
DK Ahmed Twaha,amesema takwimu za kiafya hususan katika maeneo ya
vijijini zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wanaofika
katika vituo vya afya ni wanawake na watoto hivyo wanahabari wanapaswa
kuibua mbinu kadhaa ya kunusuru kundi hilo kwa kuripoti njia bora za
kujikinga na maambukizi ya maradhi kama vile Ukimwi na Malaria.
MUSOMA
MUUNGANO wa vilabu vya waandishi wa habari nchini UTPC, umenza kutoa mafunzo maalum kuandika habari za afya kwa waandishi wa habari katika mikoa yote nchini.
Hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za afya zilizofanyiwa utafiti wa kina kwa lengo la kuboresha sekta afya na kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Mkurugenzi wa UTPC Bw Aboubakar karssan, ameyasema hayo mjini Musoma wakati wa mafunzo ya kwanza ya siku nne kuanza kutolewa nchini kwa waandishi wa habari mkoani Mara ikiwa ni sehemu ya utatuzi wa matatizo na kuibua changamoto zinazokabili utoaji wa huduma ya afya nchini.
Amesema kwa muda mrefu jamii imekuwa ikikabiliwa na sintofahamu juu ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa hususan Ukimwi kutokana na waandishi nchini kutoandika habari ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina ambao haotoi majibu ya namna ya kujikinga na maambukizi mapya.
Kwa sababu hiyo ametoa wito kwa wanahabari mkoani Mara kutumia vema nafasi ya mafunzo hayo kwa lengo la kuibua changamoto zinazokabili sekta ya afya hasa maeneo ya vijijini ili kuwezesha wananchi kutumia mbinu bora za kujikinga na maradhi.
Kwa mujibu wa mwezeshaji wa mafunzo hayo DK Ahmed Twaha,amesema takwimu za kiafya hususan katika maeneo ya vijijini zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya ni wanawake na watoto hivyo wanahabari wanapaswa kuibua mbinu kadhaa ya kunusuru kundi hilo kwa kuripoti njia bora za kujikinga na maambukizi ya maradhi kama vile Ukimwi na Malaria.
Comments
Post a Comment