TUSIWAUMIZE WENZETU KWA KUWAVISHA PETE ZA UCHUMBA
Siku mbili zilizopita nilipata message kutoka kwa rafiki yangu
ambaye ni msichana...kiukweli nilipatwa na kigugumizi cha mikono ni kwa
jinsi gani nitaweza kumshauri kwa kupitia ujumbe mfupi wa mkononi yaani sms aweze kuona kwamba swala lililomtokea ni
la kawaida kwa maana kwamba binadamu tumeumbiwa matatizo na ni jukumu
letu kupambana nayo mpaka kupata suluhisho la matatizo hayo.
Story ilikuwa hivi,dada huyu ambaye ndio rafiki yangu alinitumia message akiniambia kuwa miezi 2 iliyopita amevalishwa pete ya ndoa na mchumba wake, sasa cha kushangaza ni kwamba wamekuwa katika mahusiano na mchumba wake huyo kwa muda wa miaka 2 bila binti kujua lolote kuwa mchumba wake alishazaa na mwanamke mwingine japokuwa binti alisha muuliza mchumba wake huyo kama ana mtoto lakini jamaa alikuwa akipinga vikali kuwa hajawai na wala hana hata wa kusingiziwa, jibu ambalo lilikuwa lkimfurahisha dada huyu na pia kuambiwa kuwa yuko peke yake hana mahusiano mengine ya nje.
Utamu wenyewe wa story unaonisukuma kuandika story hii ni huu hapa .....juzi juzi Binti alikwenda kwa mchumba wake bila taarifa yoyote eeh!!!!si kufika ndo kukuta mchumba wake yuko juu ya kifua cha mwanamke mwingine.....so fumanizi likawa nimefanyika kwa dada huyo kushuhudia kitu live bila chenga. mara majibizano ya hapa na pale na purukushani zikazuka kama unavyojua tena wakati fumanizi linapotokea, hata yule mwizi naye hakujua kuwa yule bwana ni mchumba wa mtu kwa wakati huo....kumbe yule dada ambaye alikuwa na mchumba wa mtu ndiye yule yule ambaye amezaa na huyo jamaaa.
Best yangu huyu ndo kuchanganyikiwa asijue la kufanya kwa wakati huo na kilichomuumiza zaidi tayari amekwisha mtambulisha mchumba wake huyo katika familia yake...dada hana la kufanya sasa hv yuko somewhere visiwani akipunguza mawazo juu ya kilichotokea,kama ni wewe mpendwa mwanablog hii unatoa ushauri gani kwa dada yetu huyu?nini afanye kwani kusahau kwa sasa ni ngumu na mambo hayaendi kabisaaaaaaaaa.
MSAADA TUTANI USHAURI UNAHITAJIKA.
Comments
Post a Comment