Facebook yasema itainunua WhatsApp

Facebook na WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana.

Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.

WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsApp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA