NANI ANAFUGA HAWA NDEGE?? MALISA GODLISTEN ANAYO MAJIBU.

kutoka katika ukurasa wa facebook wa Malisa Godlisten nikakutana na hii, mdau fatilia kilichotabainishwa humu ndani na ndugu Malisa. 


Huu umoja wa wabunge wanaopinga ujangili ni mradi wa nani?? Umeundwa lini? Umeanza kufanya kazi lini? Umoja huu sio rasmi means hautambuliki bungeni hivyo haupati fedha yoyote kutoka bungeni za kuendesha shughuli zake. Sasa wanapata wapi fund ya kuoperate na kufanya Press conference??

Halafu wanapotoa misimamo, wanatoa misimamo kama nani? Maana kisheria mambo yote yanayohusu m...aliasili na utalii yanasemewa na kamati ya maliasili na utalii inayoongozwa na Mh.James Lembeli.

Sasa hawa wanapotoa misimamo, vp misimamo yao ikacontradict misimamo ya kamati ya maliasili na utalii ambayo ndio inayotambulika kisheria?

Halafu "kiumoja hiki" kilikuwa wapi siku zote,.mbona wasitoe matamko hadi Uingereza iliposhutumu kuwa vitendo vya UJANGILI NCHINI VINAFADHILIWA NA VIONGOZI WA SERIKALI.??

Umoja huu unaoongozwa na Rizik Said, huku wajumbe wote wakiwa ni wabunge wa CCM umeibuka na kupinga taarifa ya Uingereza na kudai eti "viongozi wa serikali wako mstari wa mbele kupambana na ujangili nchini"

Hivi kweli viongozi wa serikali wangekua mstari wa mbele kupambana na ujangili tembo wetu wangeuawa kila siku?

Halafu wanamshutumu waziri kivuli wa maliasili na utalii Mch.Msigwa kuwa eti alisaliti nchi kwa kukubali kuhojiwa na gazeti la Daily Mail la Uingereza na kueleza hali ya ujangili nchini.

Hivi Msigwa alipoeleza kuwa hali ya tembo nchini ni mbaya na kwamba tembo wanateketea.. hapo alifanya usaliti gani.? Walitaka aseme tembo nchini wanazaliana na kuongezeka kuliko nchi yoyote duniani?? Aseme Uongo, kulinda serikali ili asionekane amesaliti??

Halafu Msigwa alihojiwa akiwa na "moral authority" kama Waziri kivuli wa maliasili na utalii. Cheo kinachotambulika bungeni, nje ya bunge na kimataifa. Uingereza wanamtambua Msigwa kama waziri kivuli ndio maana wakamhoji.

Hiki kiumoja hakitambuliki hata bungeni, kinapata wapi moral authority ya kumpinga Msigwa??

Hivi huu umoja unajielewa kweli? Kama serikali imeshutumiwa, kiprotocal serikali yenyewe ndio inatakiwa ijibu sio bunge.
Kikubwa ambacho bunge lingeweza kufanya ni kuiagiza kamati ya Maliasili na utalii kuchunguza tuhuma hizo kama ni kweli wapo viongozi wa serikali wanaofadhili ujangili au lah.

Binafsi naamini Uingereza haiwezi kukurupuka kushutumu serikali yetu. Lazima wana evidence.

Bunge kama chombo kinachosimamia serikali walipaswa kufanya uchunguzi wa kina na kuja na ripoti ya kuridhisha, sio kuunda kiumoja cha "kipuuzi" cha kuisafisha serikali.

SOLUTION
1.Umoja huu ufutwe haraka iwezekanavyo kwa sababu haupo kisheria.

2.Wabunge wanaouda umoja huu wachukuliwe hatua kali za kisheria/kinidhamu kwa kuingilia kazi za kamati ya maliasili na utalii.

3.Kamati rasmi ya maliasili na utalii inayoongozwa na Lembeli wapokee taarifa ya Uingereza na kuifanyia kazi kuona kama ni kweli wapo viongozi wa serikali wanaofadhili Ujangili nchini.

4.Baada ya uchunguzi taarifa hiyo iwasilishwe bungeni na hatua zichukuiwe.

5.Wabunge wanaounda umoja huu feki, wawajibishwe na wananchi wao. Plz wananchi wa majimbo husika, make sure hawarudi bungeni mwakani coz wamewasaliti.

Nadhani hawa ni wabunge wenye njaa walioamua kusaliti wananchi kwa mlo wa siku moja. NANI ANAFUGA HAWA NDEGE.?

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA