Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga (Kulia) akiongea na waandishi wa habari, Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Laurent Shirima. Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), imeyafungia makampuni 7 pamoja na wakurugenzi wake kutokana na vitendo vya udanganyifu. Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya PPRA, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga amesema kuwa Mamlaka hiyo imeamua kuyafungia makampuni hayo kwa mujibu wa kifungu cha 62 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 na Kanuni ya 98 ya Tangazo la Serikali Na. 446 la Mwaka 2013. Aidha, Balozi Lumbanga alisema kuwa kati ya makampuni hayo, Gagaja Contractors Company Limited, limefungiwa kwa kipindi cha miaka 10 (kutoka tarehe 2 Oktoba,2015 hadi 1 Octoba, 2025) kwa kosa la kuwasilisha dhamana za zabuni za kughushi wakati wa michakato ya zabuni. Aidha, Balozi Lumbanga alisema kuwa m...