Rais Kikwete ateua Wakuu wapya wa Wilaya 13 na kuhamisha 7



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wa wilaya wapya 13 na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.

Wakuu wa wilaya 13 walioteuliwa ni Shaaban Athuman Ntanambe ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkoa wa Kagera; Thabisa Mwalapwa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara; Richard Kasesera ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Ruth Msafiri ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Mkoa wa Kigoma na Abdallah Njwayo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi.

Wakuu wa Wilaya wengine wapya ni Asumpta Mshama ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe; Mohammed Mussa Utaly ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma; Dauda Yasin ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe; Honorata Chitanda ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera; Vita Kawawa ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga na Christopher Ng’ubyagai ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida.

Wakuu wengine wapya ni Hawa Ng’humbi ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga na Mrisho Gambo ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma.

Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha; Wilson E Nkambaku ambaye anahamishiwa Arumeru, Mkoa wa Arusha kutoka Kishapu, Mkoa wa Shinyanga; Francis Miti ambaye anahama Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara kwenda Monduli, Mkoa wa Arusha na Jowika Kasunga ambaye anahamia Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa kutoka Monduli .

Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Wilaya ya Makete, Mkoa wa Njombe kwenda Wilaya ya Morogoro; Hadija Nyembo ambaye anahamia Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Tabora kutoka Uvinza, Mkoa wa Kigoma na Benson Mpyesya ambaye anahamia Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma kutoka Kahama.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

04 Oktoba, 2015

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA