Magoli ya Mbwana Samatta katika mechi dhidi ya Al Merreikh na kuifikisha TP Mazembe fainali.


         


Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya klabu ya Al Merreikh ya Sudan, huu ni mchezo wa pili wa marudiano baada ya ule wa awali kuchezwa Sudan wiki kadhaa nyuma.
28avr13-tpm-vclu_358_1367175061
Mtanzania Mbwana Samatta amesaidia timu yake kupata ushindi wa goli 3-0 katika mechi hiyo ya marudiano baada ya kufunga goli mbili dakika ya 53 na 69 kabla ya Assale kupachika goli la tatu dakika ya 71. TP Mazembe inaingia hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Al Merreikh kwa jumla ya goli 4-2 idadi ya goli hizo ni pamoja na mechi ya kwanza Sudan.
mbwana-samata-kazini
Mtanzania mwingine anayeichezea klabu hiyo Thomas Ulimwengu alipata nafasi ya kuingia dakika ya 58 ya mchezo baada ya kuchukua nafasi ya Kalaba, Ulimwengu hakupata nafasi ya kufunga goli ila alikuwa ni moja kati ya waliotengeneza goli la pili la Mbwana Samatta, sasa TP Mazembe itacheza hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria ambao watacheza fainali yao ya kwanza kihistoria baada ya kuitoa Al Hilal ya Sudan.

Baada ya mchezo huo kumalizika Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajia kuwasili Tanzania muda wowote wakitokea Congo ili kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kinachojiandaa na mechi dhidi ya Malawi October 7 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Hizi ndio video zenyewe mtu wangu



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA