NHC YAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA BIASHARA NA MAKAZI ZA MOROCCO SQUARE
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na
makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa
wiki. (Picha na Francis Dande)
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu
Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.
Wageni waalikwa.
Wageni waalikwa.
Naibu
Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia
Mchechu.
Burudani ya muziki.
Burudani ikiendelea.
Naibu
Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia
Mchechu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo.

Na Francis Dande
NAIBU
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki,
amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa kujenga
nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya makazi na biashara.
Waziri
Kairuki aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua
mauzo ya nyumba za biashara na makazi zilizojengwa eneo la Morocco
Square, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Aliwapongeza
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na wenzake kwa kazi nzuri
wanayoifanya kwa kiasi kikubwa katika kuleta uhai na taswira nzuri ya
shirika hilo.
Alisema
kuwa serikali inatambua kuwa makazi ni jambo muhimu kwa maendeleo ya
taifa, ndiyo maana imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ili kuwezersha
sekta ya nyumba kuwa endelevu na yenye tija kwa wananchi na uchumi wa
nchi.
Alibainisha
kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza sekta hii ni kuwa na
Sheria ya Mikopo ya nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision
Act) ya mwaka 2008, iliyoanzishwa kuweza kuwafanya wadau wa sekta
ya nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa nyumba na taasisi za
fedha kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta hii muhimu.
Aidha
, alisema tangu kuwapo kwa sheria hiyo, tangu mwaka 2008
kumeshuhudiwa benki 19 kati ya zaidi ya benki 50 zilizopo nchini
zikitoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania, 16 kati ya hizo zikiwa
zimesaini makubaliano na na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza
kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.
Naibu
waziri huyo alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya riba
kubwa ya mikopo ya nyumbva inayotozwa na benki mbalimbali ambayo ni
kati ya asilimia 18 na 25, serikali itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya
kuewezesha benki kupunguza riba katika mikopo ya nyumba ili
Watanzania wengi waweze kukopa na kununua nyumba.
Aliwahimiza
Watanzania kutumia fursa zilizopo za mikopo ya Benki kununua nyumba
zinazojengwa na NHC, ikiwamo kujitokeza kwa wingi kununua nyumba hizo
za za mradi wa Morocco Square ambao una nyumba za ofisi hoteli, makazi
na maduka makubwa.
chanzo:mjengwablog
Comments
Post a Comment