TRUMP ASEMA KAMPENI YAKE NI IMARA

Donald Trump
Donald Trump amekuwa akishutumiwa kwa kauli zake
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hakuna mgawanyiko kwenye kambi yake ya kampeni, licha ya taarifa kudokeza kwamba kuna mzozo mkubwa katika chama hicho.
Akihutubu katika mkutano wa hadhara Florida, Bw Trump amesema kampeni yake "inafanya vyema sana".
Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump kurejea matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanajeshi aliyeuawa nchini Iraq.
"Ningetaka kuwafahamisha tu kwamba kampeni inaendelea vyema sana," amewaambia watu waliohudhuria mkutano wake eneo la Daytona Beach.
Awali, msaidizi mkuu wake Donald Trump Paul Manaford alikuwa pia amekana taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye kampeni baada ya kile kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea huyo wa chama cha Republican, zenye kukwaza.
''Kampeni ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga mbele,'' aliiambia kituo cha runinga cha Fox News.
Baadhi ya Maafisa wa Kampeni za Trump wamesema ''wanahisi kuwa wanapoteza muda wao''.
Hata hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa Trump wa Chama cha Democratic, Hillary Clinton kwa ripoti hizo
Manafort
Bw Manafort amesema watu wengi bado wana imani na Bw Trump''Hii ni kauli nyingine ya Clinton ambayo imebebwa na vyombo vya habari, amesema ''Bwana Trump amejitokeza wiki hii kwenye mikusanyiko mikubwa sana ya watu walifurika mpaka mtaani''.
Siku ya Jumatano Bw Trump mwenyewe pia aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa ''kuna umoja kwenye Kampeni yangu, pengine mkubwa zaidi kuliko siku zote''.
Vita vyake vya maneno na Khizr na Ghazala Khan, wazazi wa Kapteni Humayun Khan aliyeuawa nchini Iraq, vimesababisha watu kutofautiana ndani ya Chama cha Republican.  
BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA