DK SLAA ATIKISA MJI WA MUSOMA LEO:
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Wilbroad Slaa leo amehutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Musoma katika uwanja wa shule ya Msingi Mukendo huku akipeleka shutuma nyingi kwa aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania Samweli Sitta. Dk Slaa aliwasili majira ya saa nane na nusu katika uwanja huo na helkopta akitokea wilayani Rorya akikuta mamia ya wakazi wa mji huo wakiwa tayari wamefika kumsikiliza,wakielezea mambo mbalimbali viongozi wa Chaema walisema kuwa muda umefika kwa utawala wa Chama cha Mapinduiz kufika kikomo. Akionyesha kuongea kwa kutoa takwimu mgombea huyo alisema kuwa kwa sasa Chama cha mapinduzi hakifanyi uchaguzi wa chama kwa chama bali ni uchaguzi kati ya Makini na tajiri huku akisema kama wananchi wataamua hakuna kinachoshindikana katika nguvu ya umma. Akionge