DK SLAA ATIKISA MJI WA MUSOMA LEO:






MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk Wilbroad Slaa leo amehutubia mamia ya wakazi wa manispaa ya Musoma katika uwanja wa shule ya Msingi Mukendo huku akipeleka shutuma nyingi kwa aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania Samweli Sitta.



Dk Slaa aliwasili majira ya saa nane na nusu katika uwanja huo na helkopta akitokea wilayani Rorya akikuta mamia ya wakazi wa mji huo wakiwa tayari wamefika kumsikiliza,wakielezea mambo mbalimbali viongozi wa Chaema walisema kuwa muda umefika kwa utawala wa Chama cha Mapinduiz kufika kikomo.

Akionyesha kuongea kwa kutoa takwimu mgombea huyo alisema kuwa kwa sasa Chama cha mapinduzi hakifanyi uchaguzi wa chama kwa chama bali ni uchaguzi kati ya Makini na tajiri huku akisema kama wananchi wataamua hakuna kinachoshindikana katika nguvu ya umma.

Akiongelea suala la Mwenge wa Uhuru Dk Slaa alisema kuwa kipindi Baba wa Taifa Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere anauibuni Mwenge huo lengo lilikuwa ni kuleta matumaini pasipo na matumaini mwanga pasipo na mwanga lakini leo Mwenge huo hauleti matumaini bali unashibisha matumbo ya wachache.

Akishangiliwa na umati wa wananchi waliojitokeza katika uwanja huo Dk Slaa alisema kuwa kama atapata ridhaa ya wananchi kuna kila sababu Mwenge huo kupelekwa katika jumba la Makumbusho kwani kwa sasa umeonekana kutoleta matumaini kwa watanzania walio wengi.


Slaa alisema kuwa umaskini wa watanzania unatokana na watanzania kuwa na elimu duni hivyo kama atafanikiwa kupata ridhaa ya watanzania basi anaimani suala la elimu litakuwa la kwanza kwani ndio njia ya kumukomboa mtanzania,alisema kwa ilani ya chama chake elimu itakuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita.

Aidha katika mkutano huo Dk Slaa alimshukia Spika aliyemaliza muda wake Samwli Sitta kuwa aache unafiki linapokuja suala la kitaifa
‘Wewe acha unafiki, Sitta ndio ulizima fedha za uuma zilizoliwa kupitia Richmond ni fedha za watanzania ambazo ulizizima bungeni” alisema Dk slaa huku akishangiliwa na wananchi na wapenzi wa chama hicho.

Alisema kuwa Sitaa alikuwa waziri katika serikali ya mwalimu Julius Nyerere na wakati huo elimu ilikuwa bure na hata yeye alisoma bure iweje leo asimame na kusema kuwa hao wanaosema kuwa wataleta elimu bure mbona katika serikali ya mwalimu iliwezkana? Alihoji Dk Slaa

Aliongeza kuwa mwaka jana wakati anapambana na ufisadi bungeni wa bilioni 30 ambazo serikali ya Mapinduzi inatumia kwa Chai Sitta alimwambia akae chini wakati yeye akiwa anatete watanzania ambao kila siku wanatozwa kodi.

Mgombea huyo alisema kuwa takwimu zinazoonyeshwa leo nje ya bunge si sahihi kwani sehemu pekee ya kuonyesha takwimu hizo ilikuwa ni bungeni,tunajua serikali ya Kikwete ni bingwa wa kutoa Takwimu kwa wananchi.Mbali na hivyo Slaa aliuliza kuhusu Meremeta,Tangold ambapo hiyo nayo Sitaa alimwambia kaa chini iweje leo aanze kusema hayo nje ya Bunge

Akiongelea mishahara ya wabunge Dk Slaa alisema ni wizi wa mchana ambapo hata spika Sitta alishiriki sasa badala ya kuweka suala hilo hadharani yeye anasema Slaa kaa chini,nasema Sitta acha unafiki.

Usafiri wa Dk Slaa na makada wake


picha ni kutoka kwenye blog ya www.mwanawaafrika.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA