Posts

MAMBO YANAVYOENDELEA NDANI YA DIAMOND JUBILEE

Image
leo ndio siku ya mwisho ya maonyesho haya ya 7 ya vyuo vikuu hapa Diamond Jubilee,so karibuni sana watu waote katika banda la St.Augustine university of Tanzania.

TOTO YAENDELEA KUGAWA DOZI ZA JIONI YAWANYWESHA AFRICAN LYON 3.

Image
Mara baada ya kutembeza kichapo cha 3-2 kwa Yanga mwishoni mwa wiki Toto Africans ya jijini Mwanza leo tena imeendeleza wimbi lake la kugawa dozi za jioni ikijitengenezea mazingira mazuri kuukwepa mstari wa hatari wa kushuka daraja mara baada ya kuizabua African Lyon ya jijini Dar es salaam bao 3-0 katika dimba lake la CCM Kirumba Mwanza.   Madaktari wa wakimpatia tiba beki wa Toto Africans aliyeumia kwenye paji lauso na kuvuja damu nyingi mara baada ya kugongana na mchezaji wa Lyon katika mchezo wa ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara leo.   Wakiliandama lango la Lyon na kucheza kufa na kupona Toto walianza mbio zao za kuusaka ushindi kwa goli safi la dakika ya 12 mfungaji akiwa Mussa Said Mussa aliyepokea pande safi toka kwa winga aliyekuwa akihaha uwanja mzima Emma Swita. Mara baada ya bao hilo African Lyon ilirejea kwenye mchezo lakini mashuti ya wachezaji wake Hassan Goboso na Benedict Jackob hayakuwa na macho kuziona nyavu za Wanakishamapanda. Wakati wapenzi wa kandanda wak

MAONYESHO YA VYUO VIKUU YAFUNGULIWA RASMI DIAMOND JUBILEE

Image
Maonyesho ya vyuo vikuu yamefunguliwa rasmi leo 18/4/2012 na Mh.Makamu wa Rais Bw.Gharib Bilal katika ukumbi wa Diamond Jubilee yatakayofanyika hadi tarehe 20/4/2012,Maonyesho haya yamelenga zaidi kuiwezesha jamii kupitia elimu ya juu,sayansi,technolojia na ugunduzi wa mambo mbalimbali. Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionyesha chuo cha Mt.Augustino kilivyojiandaa katika maonyesho haya . Mgeni rasmi Mh.Dr.Gharib Bilal makamu wa Rais wa Tanzania akiwa meza kuu tayari kufungua maonyesho. Francis,Kisaka,Nyanja wakichakarika kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Lucky Mgimba akitoa maelezo mbalimbali yanayohusiana na sheria Aidan Kaijanante akitoa maelezo mbalimbali kwa watembeleaji wa banda la SAUT Blogger mwenyewe nikiwepo pia kuwakilisha chuo changu . Watembeleaji wa Banda la SAUT Veneranda Kessy pia yupo kuakikisha mambo yanaenda sawa. Komu living pamoja na Alda Sadango wakitoa huduma kwa watembeleaji wa banda la Saut Loi Kababa akifafa

Bibi Cheka toka TMK Wanaume ndani ya kili music awards 2012

Image

DIIAMOND ANG'ARA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS.

Image
 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utuzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora za Kilimanjaro Music Award 2012 zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi, Diamond amejipatia tuzo tatu kwa mpigo.   Msanii huyo ameibuka kidedea katika tuzo ya mtunzi bora , mtayarishaji bora wa mwaka na tuzo ya Video bora ya Mwaka  Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzi bora wa nyimbo.  Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu

KILIMANJARO MUSIC AWARDS WILL BE SHOWN ONLINE

Streaming video by Ustream

MR BLUE MALAYSIA TOUR

Image

Magazetini ya Leo, "Ni Lulu" tu

Image

MIIKO YA UANDISHI MBONA HAIFUATWI?

Kuna maswali mengi nimekuwa nikijiuliza hasa pale napoona picha zisizotakiwa kutolewa kwa kuchapichwa kwenye magazeti au katika vyombo mbalimbali vya habari kwa kuwa vinakuwa vimekiuka miiko ya uandishi wa habari(media ethics) hasa kwenye upande wa photojournalism. Picha nyingi zimechapishwa kwenye magazeti yetu zikionyesha mwili wa marehemu Steven Kanumba akiwa mochwari na zingine akiwa kwenye sanduku,bila aibu watu hawa ambao ni waandishi wa habari waliosomea na wanajua maadili na miiko ya uandishi lakini bado ndio wanaozichapisha picha hizo tena kwenye ukurasa wa mbele. Kuna baadhi ya watu hauwezi kuwalaumu hasa wanaotumia mitandao ya kijamii kwani kwa upande wao wanaona ni kawaida na hakuna tatizo lolote,kwani hawajui miiko ya uandishi wa habari,lakini swala la msingi linakuja pale mwandishi ambaye amesomea taaluma ya uandishi wa habari naye anadiliki kutoa picha hizo tena kwenye ukurasa wa mbele kabisa wa gazeti. Baraza la habari lipo wapi? wanaliangalia swala hili na kul

ARSENAL, MANCHESTER CITY WAPETA, MAN UTD WAPOTEZA MECHI YAO

Image
Wachezaji wa Manchester City David Silva (kushoto), Sergio Aguero (wa pili kushoto) and Carlos Tevez (kulia) wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Sergio Aguero wakati wa mechi yao na West Bromwich Albion leo. (Picha na Adrian Dennis/AFP/Getty Images). Kiungo wa Arsenal, Alex Song (kushoto) akiwania mpira na kiungo wa Wolverhampton Wanderers, Nenad Milijas (kulia) wakati wa mechi yao. (Picha na Ben Stansall/AFP/Getty Images). Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (kulia) akimpa maelekezo mshambuliaji wa timu hiyo Wayne Rooney wakati wa mechi yao dhidi ya Wigan leo.

UZINDUZI WA MIXTAPE YA NASH EMCEE TAREHE 21 APRIL

Image
KUWA WA KWANZA KUJIPATIA NAKALA YAKO YA MZIMU WA SHAABAN ROBERT, KANDAMSETO KUTOKA KWA NASH EMCEE, SIKU YA TAREHE 21/04/2012 PALE BAMAGA/KIJITONYAMA NDANI YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KIINGILIO NI BURE ILA CD ITAPATIKANA KWA SHILINGI ZA KITANZANIA ELFU SITA (6000/=)

DHAMANA KESI ZAO ZAANZA KUUNGURUMA MAHAKAMANI

Image
TWENTY PERCENT ASAFIRI KWENDA CONGO NA KUSHINDWA KUHUDHURIA MAHAKAMANI WAPANGA KUZIHAMISHA KESI HIZO KUTOKA MAHAKAMA ZA MWANZO KWENDA KTK LEVEL YA MAHAKAMA YA WILAYA AU MKOA ILI WAWEZE KUMSIMAMISHA MWANASHERIA AWATETEE  Afande Sele KATIKA ZILE KESI TANO ZINAZOWAKABILI WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AFANDE SELE, TWENTY PA PAMOJA NA WENZAO WAWILI, OF COZ UTAKUA UNAIKUMBUKA NI ILE AMBAYO WALIDAIWA KUINGIA TOWN WAKIWA WAMETUPIA VICHUPI, KUFANYA FUJO, KUJERUHI N.K JANA ILITAJWA MOJA WAPO NA KESHO KESI NTYINGINE ITA TAJWA, ILA KATIKA KESI HIZO MSANIIN TWENTY PA ATASHINDWA KUHUDHURIA MAHAKAMANI MPAKA ATAKAPO REJEA KUTOKA NCHINI CONGO ALIKOKWENDA KWA AJILI YA KUTUMBUIZA, HIVYO AMEOMBA RUHUSA MAHAKAMANI. AFANDE SELE NA WENZAKE WANAPANGA KUFUATA HATUA ZA KISHERIA ILI KESI YAO IHAMISHWE KUTOKA MAHAKAMA ZA MWANZO NA IENDE KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA AU MKOA ILI WAWEZE KUSIMAMISHA MWANASHERIA WA KUWATETEA.