TOTO YAENDELEA KUGAWA DOZI ZA JIONI YAWANYWESHA AFRICAN LYON 3.

Mara baada ya kutembeza kichapo cha 3-2 kwa Yanga mwishoni mwa wiki Toto Africans ya jijini Mwanza leo tena imeendeleza wimbi lake la kugawa dozi za jioni ikijitengenezea mazingira mazuri kuukwepa mstari wa hatari wa kushuka daraja mara baada ya kuizabua African Lyon ya jijini Dar es salaam bao 3-0 katika dimba lake la CCM Kirumba Mwanza.  
Madaktari wa wakimpatia tiba beki wa Toto Africans aliyeumia kwenye paji lauso na kuvuja damu nyingi mara baada ya kugongana na mchezaji wa Lyon katika mchezo wa ratiba ya ligi kuu soka Tanzania bara leo.
 
Wakiliandama lango la Lyon na kucheza kufa na kupona Toto walianza mbio zao za kuusaka ushindi kwa goli safi la dakika ya 12 mfungaji akiwa Mussa Said Mussa aliyepokea pande safi toka kwa winga aliyekuwa akihaha uwanja mzima Emma Swita.

Mara baada ya bao hilo African Lyon ilirejea kwenye mchezo lakini mashuti ya wachezaji wake Hassan Goboso na Benedict Jackob hayakuwa na macho kuziona nyavu za Wanakishamapanda.

Wakati wapenzi wa kandanda wakiamini kuwa kipindi cha kwanza kitayeyuka kwa matokeo yaleyale ilikuwa ni dakika ya 43 Iddy Moby aliyeitumia vyema pasi ya Mnaigeria Enyina Darlington kwa kuipatia Toto goli la pili. Hadi mapumziko Toto ilikuwa inaongoza goli 2 - 0.

Kasi ya mchezo ilirejea upya kipindi cha pili kwa pande zote mbili kushambuliana na kucheza kandanda salfi la kuonana. Hatimaye mwiba wa mwisho kwenye jeraha la Africa Lyon ukashindiliwa na Salum Kamana aliyefunga katika dakika ya 87 ya mchezo.

Hadi Mwisho wa game Toto 3 African Lyon 0.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA