DIIAMOND ANG'ARA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS.

 Mwanamuziki Diamond (kulia)akipokea tuzo yake kutoka kwa George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro mara baada ya kutangazwa mshindi wa utuzi bora wa nyimbo katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora za Kilimanjaro Music Award 2012 zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi, Diamond amejipatia tuzo tatu kwa mpigo.
 
Msanii huyo ameibuka kidedea katika tuzo ya mtunzi bora , mtayarishaji bora wa mwaka na tuzo ya Video bora ya Mwaka
 Mwanamuziki Diamond akipiga picha na mama yake wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kutoka kulia pamona na wanenguaji wake mara baada ya kupokea tuzo yake ya utuzi bora wa nyimbo.
 Mwimbaji wa muziki wa Taarab ambaye ameshinda tuzo ya mburudishaji bora kwa wanawake Malkia Khadija Omar Kopa akitumbuiza katika hafla hiyo usiku huu.
 Malkia Khadija Omar Kopa akishukuru wapenzi wake mara baada ya kushinda tuzo ya mburudishaji bora, wa pili kutoka kushoto ni mume wake na wengine ni watoto wake.
 Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani mara baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.
 Kulia ni Msanii Profesa Jay na kushoto ni Mkubwa Fella meneja wa kundi la TMK Family wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.

 Burudani kutoka THT
 Burudani zikiendelea kwa nguzu zote.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA