MIIKO YA UANDISHI MBONA HAIFUATWI?

Kuna maswali mengi nimekuwa nikijiuliza hasa pale napoona picha zisizotakiwa kutolewa kwa kuchapichwa kwenye magazeti au katika vyombo mbalimbali vya habari kwa kuwa vinakuwa vimekiuka miiko ya uandishi wa habari(media ethics) hasa kwenye upande wa photojournalism.

Picha nyingi zimechapishwa kwenye magazeti yetu zikionyesha mwili wa marehemu Steven Kanumba akiwa mochwari na zingine akiwa kwenye sanduku,bila aibu watu hawa ambao ni waandishi wa habari waliosomea na wanajua maadili na miiko ya uandishi lakini bado ndio wanaozichapisha picha hizo tena kwenye ukurasa wa mbele. Kuna baadhi ya watu hauwezi kuwalaumu hasa wanaotumia mitandao ya kijamii kwani kwa upande wao wanaona ni kawaida na hakuna tatizo lolote,kwani hawajui miiko ya uandishi wa habari,lakini swala la msingi linakuja pale mwandishi ambaye amesomea taaluma ya uandishi wa habari naye anadiliki kutoa picha hizo tena kwenye ukurasa wa mbele kabisa wa gazeti.

Baraza la habari lipo wapi? wanaliangalia swala hili na kulinyamazia kimya bila kuchukua hatua zozote za kisheria kwa wale wanaoenda kinyume na taratibu za uandishi?ndio maana imefikia hatua hata picha zisizokuwa na maadili zinatolewa tu kila kukicha kwenye magazeti.

Kama mlikuwa hamfahamu mwili wa marehemu au viungo vyoyote vya binadamu ambaye anakuwa amepata ajali mfano mguu, mkono,nk havipaswi picha zake kuchapichwa wala kuonyeshwa na kwa kufanya hivyo unakuwa umekiuka miiko ya uandishi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA