Posts

Hussein Machozi afanya ngoma na mwanadada Size 8 wa Kenya

Image
Mwanamuziki wa Tanzania Hussein Machozi amefanya ngoma na msanii wa kike Size 8 anayetemba sana kwa sasa nchini Kenya pamoja na Afrika Mashariki. Wimbo huo ambao umefanyika katika studio za Ogopa Djs za nchini humo unaitwa Addicted. Machozi anasema wimbo huo ni kwaajili ya mashabiki wake wa kike ambapo video ya wimbo huo itafanywa na kampuni ya Ogopa DJs. Kwa sasa Size 8 ambaye jina lake halisi ni Linet Masiro Munyali anakimbiza na club banger yake iitwayo Vidonge. Mwaka jana msanii huyo alitajwa kuwania tuzo za Chagua La Teeniez za Kenya kwenye kipengele cha mwanamuziki bora wa kike. Hii si mara ya kwanza kwa Hussein Machozi kumshirikisha msanii wa Kenya kwani tayari ana wimbo alioufanya na mwanadada Habida uitwao Asante.

WAUGUZI WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA WAGOMA

Augustine Mgendi Wauguzi katika hospitali ya Mkoa wa Mara wameweka mgomo wa kuingia wodini na kutoa huduma mbalimbali katika hospitali hiyo wakishinikiza uongozi wa hospitali hiyo kuwalipa madai yao mbalimbali ambayo wanadai na kusema kuwa hawatafanya kazi mpaka hapo watakapo tekelezewa. Mgomo huo wa wauguzi umeanza leo asubuhi baada ya wauguzi hao kufika kazini na kushindwa kufanya kazi huku wakisema kuwa wamenyanyaswa vya kutosha na wanachotaka nikulipwa madai yao ndipo huduma kutoka kwao ziweze kuendelea katika hospitali hiyo. Kutokana na mgomo huo kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa wa wodini na wale wa nje baada ya kukosa huduma mbalimbali huku wengine wakitupia lawama kwa uongozi wa hospitali hiyo kwa kushindwa kukaa na wauguzi hao na kufika muafaka ili waendelelee kupata huduma kama kawaida. Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo Antunia Machibula alisema kuwa kutokana na kushindwa kuthaminiwa kutokana na kupuuzwa kwa malipo yao na shughuli wanazozifanya wameamua

HUKUMU YA JOHN MNYIKA LEO...

Image
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,John Mnyika. NI KATIKA HUKUMU YA KESI KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE WA JOHN MNYIKA James Magai MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, leo itawaliza au kuwafurahisha wapenzi na wanachama wa Chadema wakati itakapotoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia chama hicho, John Mnyika. Kesi hiyo namba 107 ya 2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ngh’umbi dhidi ya Mnyika ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo akitetewa na Wakili Edson Mbogoro. Mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo iliyoko mbele ya Jaji Upendo Msuya ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi (RO) katika jimbo hilo, (aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni) ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA), Justice Mulokozi. Katika uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 31, 2010, Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi Novemba 2, 2010 baada ya kupata kura 66,742. Ngh

KANYE WEST NA BEYONCE WAONGOZA KATIKA KUWANIA TUZO ZA BET 2012

Image
Majina ya wanaowania tuzo za BET kwa mwaka 2012 yamewekwa wazi. Wanaoongoza kwa kuteuliwa kuwania tuzo nyingi ni Beyonce aka Mrs Jigga na shemejie Kanye West.Wakati Beyonce anawania tuzo 6,Kanye anawania 7. Washindi wa tuzo za BET mwaka huu watatangazwa katika show maalumu itakayofanyika tarehe 1 Julai kutokea Shrine Audotorium huko Los Angeles. Mwigizaji maarufu, Samuel L.Jackson ndiye atahost show ya mwaka huu. Hii hapa chini ni orodha kamili ya walioteuliwa kuwania tuzo hizo na vipengele vyake Best Female R&B Artist Marsha Ambrosius Beyoncé Mary J. Blige Melanie Fiona Rihanna Best Male R&B Artist Chris Brown Bruno Mars Miguel Trey Songz Usher Best Male Hip-Hop Artist Big Sean Drake J. Cole Lil Wayne Rick Ross Young Jeezy Best Female Hip-Hop Artist Nicki Minaj Diamond Trina Brianna Perry

VIMWANA MISS NYAMAGANA HAWA HAPA!!!

Image
Shindano la Miss Nyamagana 2012, Litafanyika katika ukumbi wa Gold Crest Mwanza, tarehe 02/06/2012 ambapo wasanii Linah, Ditto na Hafsa Kazinja watalipamba jukwaa. Mc katika shindano hilo ni msanii maarufu katika tasnia ya uchekeshaji na mzungumzia Mpoki. Jumla ya warembo 20 watapanda jukwaani kumpata Miss Nyamagana 2012, kabla ya shindano la kumpata mrembo wa Mkoa wa Mwanza. Katika mahojiano yaliyofanyika, warembo wameonekana kuwa na shauku kubwa ya ushindi, wakiaahidi kurudisha taji la Miss Tanzania Mkoani Mwanza. Shndano la Miss Nyamagana 2012 linaandaliwa na Stoppers Entainment ya jijini Mwanza. Vimwana wakipata flash.. Vimwana wa Nyamagana na flash...   SOURCE www.gsengo.blogspot.com  

Redds Miss Chan'gombe hiyooo yaja!!

Image
  Wanyange wanaowania taji la Redds Miss Cha'gombe 2012 wakiwa katika picha ya pamoja iliyopigwa muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi yao jana katika ukumbi wa TCC Chan'gombe jijini Dar es Salaam. Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012.

MADEREVA WA BODABODA MJINI MUSOMA WAPEWA SOMO

Na Shomari Binda Musoma, Madereva wa pikipiki zinazobeba abiria maarufu kama bodaboda mjini Musoma wametakiwa kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaweza kusababisha vifo na majeruhi kwa abiia na waendeshaji wa pikipiki na hivyo kusababisha kupunguza nguvu kazi ya Taifa. ... Kauli hiyo imetolewa na muuzaji na msambazaji wa pikipiki aina ya Toyo Mjini hapa Seif Pazi alipokuwa akizungumza na madereva wa pikipiki katika viwanja vya Shule ya msingi Mukendo katika kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia sheria wawapo barabarani na kusema katika ufatiliaji uliofanywa na wadau mbalimbali wa usalama barabarani umebaini ajali nyingi nyingi za pikipiki zinatokana na kutokuzingatia sheria. Alisema ajali nyingi zinaweza kuepukika iwapo madereva watakuwa makini pindi waendeshapo vyombo vyao na kuvifanyia uchunguzi wa mara kwa mara ili kuweza kuvifanyia matengenezo kwa vile vinavyohitaji matengenezo kwani kwa kufanya hivyo kutapel

Waziri Akumbana Na Madudu Maliasili

Image
 WAZIRI mpya wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ameelezea kushtushwa kwake na ubadhilifu wa kutisha ulioko katika wizara hiyo, Idara ya Wanyamapori unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji wake.   Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) jijini Dar es Salaam, jana, waziri huyo alisema idara hiyo inanuka kwa uozo unaotokana na wizi na ubadhilifu mkubwa ambao umeleta hasara kwa taifa.   Kagasheki alidai idara hiyo inaongoza kwa madudu ya kutisha, na ametangaza kuchukua hatua za haraka dhidi ya watendaji wanaotuhumiwa kuhusika na ubadhilifu huo mkubwa haraka iwezekanavyo, akidai fedha zilizotafunwa na wajanja hao ni nyingi.   “Jamani Idara ya Wanyamapori ina fedha nyingi, lakini zinaliwa na watu kwa maslahi binafsi, na kama fedha hizo zingekuwa zinapelekwa serikalini kama inavyohitajika, nchi hii kwa sasa ingefika mbali, mimi

Ajari Mbaya Yatokea Iringa

Image
Askari wa usalama barabarani mjini Iringa wakiwa wamebeba moja kati ya maiti za ajali ya Taxi na Fuso iliyotokea eneo la kituo cha Mafuta Eso kwenye barabara kuu ya Iringa -Mbeya asubuhi hii Wananchi wakitazama Fuso ambalo liligongana na Taxi hiyo Miili ya wafanyakazi wa barabara Iringa ambao walikufa katika ajali hiyo Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali Hivi ndivyo Fuso hilo lilivyokuwa baada ya ajali Mwili wa dereva Taxi ukiwa bado kutolewaAjali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo huku abiria waliokuwemo katika fuso wakinusurika katika ajali hiyo .   source www.freebongo.blogspot.com

picha: Annular Eclipse, May 2012

Image
 Ni nadra kuona "annular eclipse" ambapo mduara unaotokana na miale ya mwanga wa jua la machweo huonekana kuuzunguka mwezi ambao kwa wakati huo ndiyo unakuwa ukichomoza na kupita kati ya jua na sayari ya Dunia. Tofauti na kupatwa kabisa kwa jua (total solar eclipse), kwenye 'annular eclipse' mwezi huwa na umbo dogo linaloshindwa kulifunika jua lote, hivyo ile sehemu ya jua inayobaki bila kuzibwa, mwanga wake ndiyo unaoonekana kuuzunguka mwezi na kutengeneza mduara wenye mfano na umbo la pete. Juzi ilitokea "annular eclipse" na baadhi ya vyombo vya habari viliwakumbusha watu kubeba zana zao za kukinga macho na kisha kushuhudia hali hyo ambayo ni nadra sana kutokea. Jumapili, annular eclipse ilishuhudiwa magharibi mwa Texas, Arizona, Oregon bahari ya Pasifiki hadi Tokyo, Japan. Picha hizi na nyingine zaidi zipo katika tovuti ya  boston.com/bigpicture                                   A composite of im

"The Spear" depicting Jacob Zuma with genitalia in the open has been vandalized

Image
                         image: zapiro.com A painting supposedly of South Africa’s President Jacob Zuma showing his genitals and the subject of a court challenge by the ruling African National Congress party has been defaced at a Johannesburg gallery. Two men smeared paint on the portrait, known as “The Spear,” which depicts Zuma in black, yellow and red in a pose similar to one in which former Russian leader Vladimir Lenin was frequently shown in Soviet propaganda posters, footage broadcast on eNews Channel showed today. The South Gauteng High Court was to hear an application to have it removed after the ANC said it infringes on Zuma’s constitutional right to dignity and privacy. The party will continue with its application on principle as the president had been humiliated, spokesman Jackson Mthembu said in an interview. ANC supporters gathered outside the court to protest against the portrait. The South African Communist Party an

Rais Kikwete ateua majaji wa Mahakama ya RUfani

T AARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani. Walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012. Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000. Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004. Imetolewa na: Kurugenz