MADEREVA WA BODABODA MJINI MUSOMA WAPEWA SOMO

Na Shomari Binda
Musoma,

Madereva wa pikipiki zinazobeba abiria maarufu kama bodaboda mjini Musoma wametakiwa kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaweza kusababisha vifo na majeruhi kwa abiia na waendeshaji wa pikipiki na hivyo kusababisha kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
...
Kauli hiyo imetolewa na muuzaji na msambazaji wa pikipiki aina ya Toyo Mjini hapa Seif Pazi alipokuwa akizungumza na madereva wa pikipiki katika viwanja vya Shule ya msingi Mukendo katika kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia sheria wawapo barabarani na kusema katika ufatiliaji uliofanywa na wadau mbalimbali wa usalama barabarani umebaini ajali nyingi nyingi za pikipiki zinatokana na kutokuzingatia sheria.

Alisema ajali nyingi zinaweza kuepukika iwapo madereva watakuwa makini pindi waendeshapo vyombo vyao na kuvifanyia uchunguzi wa mara kwa mara ili kuweza kuvifanyia matengenezo kwa vile vinavyohitaji matengenezo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea kuepusha ajali ambazo si za lazima.

Alidai wapo madereva na wamiliki wa pikipikia ambao wanashindwa hata kuvifanyia marekebisho vyombo vyao vya usafiri kwa muda mrefu na wengine hata kushindwa kubadilisha taa zilizoungua na matokeo yake kushindwa kutoa muelekeo mzuri barabarani na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuepukika.

"Sisi kama wasambazaji na wauzaji wa pikipiki za Toyo tumeona tuna wajibu kutoa elimu kwa madereva na kuhamasisha matengenezo ya vyombo na kuwafanyia matengezezo madogo ikiwa ni kuhamasisha ili nao waweze kuona umuhimu wake ili kuweza kupunguza ama kumaliza kabisa ajali za barabarani zitokanazo madereva wa pikipiki zinazobeba abiria",alisema Pazi.

Alisema licha ya kutoa elimu hiyo ya kuzingatia sheria barabarani na kufanya matengenezo ya pikipiki pia wamegawa kufia za kuendeshea zaidi ya 500 kwa madereva na kuwataka kuzingatia uvaaji wa kofia hizo pindi waendeshapo wakiwa na abilia kwani ni muhimu katika kujali maisha.

Aidha Pazi aliwaomba wadau wengine wa usalama barabarani kutokuchuka kutoa elimu kuhusiana na waendeshaji wa pikipiki ili kuweza kupunguza ajali zitokanazo na usafiri huo ambao kwa sasa unatumiwa na wananchi wengi katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na utafutaji.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA