WAUGUZI WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA WAGOMA
- Get link
- X
- Other Apps
Wauguzi
katika hospitali ya Mkoa wa Mara wameweka mgomo wa kuingia wodini na
kutoa huduma mbalimbali katika hospitali hiyo wakishinikiza uongozi wa
hospitali hiyo kuwalipa madai yao mbalimbali ambayo wanadai na kusema
kuwa hawatafanya kazi mpaka hapo watakapo tekelezewa.
Mgomo
huo wa wauguzi umeanza leo asubuhi baada ya wauguzi hao kufika kazini
na kushindwa kufanya kazi huku wakisema kuwa wamenyanyaswa vya kutosha
na wanachotaka nikulipwa madai yao ndipo huduma kutoka kwao ziweze
kuendelea katika hospitali hiyo.
Kutokana na mgomo huo
kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa wa wodini na wale wa nje
baada ya kukosa huduma mbalimbali huku wengine wakitupia lawama kwa
uongozi wa hospitali hiyo kwa kushindwa kukaa na wauguzi hao na kufika
muafaka ili waendelelee kupata huduma kama kawaida.
Mmoja wa
wauguzi wa hospitali hiyo Antunia Machibula alisema kuwa kutokana na
kushindwa kuthaminiwa kutokana na kupuuzwa kwa malipo yao na shughuli
wanazozifanya wameamua kufanya hivyo ili kushinikiza kulipwa malipo yao
wanayoyadai na kusema kuwa malipo wanayodai tayari yalishatolewa kutoka
katika ofisi za ngazi ya juu zinazohusika.
Amesema kuwa baada
ya kutokea mgomo wa madaktari miezi michache iliyopita ofisi ya Waziri
Mkuu ilifanya malipo yote yanayohusiana na madaktari na waauguzi lakini
cha kushangaza wao wameshindwa kulipwa huku wengine wakilipwa kiwango
ambacho akistahili katika malipo yaliyokuwa yamekokotolewa.
"Kwa mfano yule muuguzi ambaye anatakiwa kulipwa malipo ya ziada ya
shilingi elfu kumi analipwa shilingi elfu tano na yule anaetakiwa
kulipwa shilingi shilingi elfu ishilini analipwa elfu kumi sasa hii
sisis tunaona ni manyanyaso kwetu na tunaomba jamii ituelewe hivyo
maana tumechoka kunyanyaswa",alisema Machibula.
Kwa upande
wake muuguzi Juma Warioba alisema kuwa ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa
kiasi cha shilingi milioni 40 kutokana na madai mbalimbali yanayowahusu
lakini wanashangazwa na kutokulipwa kama inavyostahili licha ya kukaa
vikao mbalimbali kuzungumzia suala hilo na kilichobaki ni kutokufanya
kazi mpaka pale madai yao yatakaposikilizwa.
Baada ya maelezo
hayo ya wauguzi wa hospitali hiyo ya Mkoa wa Mara kueleza madai yao
BINDA NEWS lilifika katika ma wodi ya hospitali hiyo na kukuta wagonjwa
wakiwa pekee yao huku kukiwa hakuna huduma mbalimbali zinazoendela za
kimatibabu na kulalamikia kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika
hospitali hiyo.
Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika
wodi namba saba aliyejitambulisha kwa jina la Musa Mikidadi alisema
tangu asubuhi ajapata huduma yeyote licha ya kutakiwa kupata huduma
kutwa mara tatu na kudai kuwa kuna mmoja wa wagonjwa jamaa zake
walilazimika kumtoa nje ya wodini na kwenda kutibiwa katika vituo
binafsi.
Sakata lingine likatokea katika chumba cha kuhifadhi
maiti katika hospitali hiyo baada ya muhudumu wa chumba hicho nae
kuweka mgomo wa kutoa wala kupokea maiti katika chumba hicho kwa kuwa
kufanya hivyo ni sawa na kuwasaliti wenzake kwa kuwa wote wapo katika
mgomo wa madai ya kimaslahi.
Muhudumu huyo aliyejitambulisha
kwa jina la Masatu Masatu alisema kuwa hataweza kufanya kazi yeyote
mpaka hapo utakapapatikana muafaka ambao wanaudai kutoka kwa viongozi
licha ya kuwepo kwa watu waliokuwa wakihitaji huduma ya kuwatoa ndugu
zao katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti.
Kutokana na
sakata hilo kulipikea katibu tawala wa wilaya ya Musoma ambaye ni kaimu
mkuu wa Wilaya ya Musoma kufika katika hospitali hiyo akiwa na kamati
ya ulinzi na usalama ya Wilaya Debora Makinga ili kuzungumza na wauguzi
hao lakini hadi majira ya saa 8;40 alasiri kulikuwa hakujapatikana
muafaka wowote kati ya wauguzi na viongozi hao.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment