DIAMOND NA JOKATE WAMWAGANA
PENZI motomoto kati ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Mrembo Nambari 3 wa Tanzania 2006, Jokate Mwegelo limedaiwa kuvunjika Kwa mujibu wa chanzo chetu, raia wa Tanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabit Manka anatajwa kuwa chanzo cha penzi la wawili hao kusambaratika. Awali, Thabit aliwahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba ‘anatoka’ na Jokate, madai ambayo kwa upande wake mrembo huyo aliyakanusha vikali akisema anasingizwa licha ya kujikanyaga katika maelezo yake. Hata hivyo, baadaye wawili hao ikasemekana wamemwagana kwa sababu ambazo hazikuwa wazi kwa vile uhusiano wao ulikuwa wa siri kubwa. Safari hii, kwa mujibu wa chanzo chetu, Hasheem amemrudia Jokate kwa nguvu zote huku ikidaiwa kwamba hitimisho la uhusiano wao litaishia kwenye kufunga ndoa na kuishi kama mke na mume. Sosi mmoja alimjulisha paparazi wetu kwa staili ya kumuuliza swali kama anafahamu lolote kuhusu wapenzi hao kupeana mkon