DIAMOND NA JOKATE WAMWAGANA
Kwa mujibu wa chanzo chetu, raia wa Tanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani, Hasheem Thabit Manka anatajwa kuwa chanzo cha penzi la wawili hao kusambaratika.
Awali, Thabit aliwahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba ‘anatoka’ na Jokate, madai ambayo kwa upande wake mrembo huyo aliyakanusha vikali akisema anasingizwa licha ya kujikanyaga katika maelezo yake.
Hata hivyo, baadaye wawili hao ikasemekana wamemwagana kwa sababu ambazo hazikuwa wazi kwa vile uhusiano wao ulikuwa wa siri kubwa.
Safari
hii, kwa mujibu wa chanzo chetu, Hasheem amemrudia Jokate kwa nguvu
zote huku ikidaiwa kwamba hitimisho la uhusiano wao litaishia kwenye
kufunga ndoa na kuishi kama mke na mume.
Sosi mmoja alimjulisha paparazi wetu kwa staili ya kumuuliza swali kama anafahamu lolote kuhusu wapenzi hao kupeana mkono wa kwaheri.
“Hivi jamani mnajua kama Jokate na Diamond wamemwagana? Demu amerudiana na Hasheem Thabit, tena safari hii watafunga ndoa kabisa,” alisema sosi huyo.
Akazidi kudai kuwa mbaya zaidi, Jokate amekata waya wa mawasiliano kati yake na Diamond, hali ambayo inampa wakati mgumu jamaa kwani uhusiano wao umevunjika huku akiwa bado anampenda.
Ili kupata uhakika wa madai haya, paparazi wa Risasi alimsaka Diamond kwa njia ya simu ambapo alipopatikana na kuulizwa kuhusu madai hayo, alikuwa na haya ya kusema:
“Hamna, hamna kitu kama hicho. Unajua mambo kama hayo msiandike. Mimi nitaondoka keshokutwa kwenda kufanya shoo Big Brother, si umesikia?”
Paparazi: Yeah! Tumesikia, habari tayari ipo kwenye gazeti.
Diamond: Basi ndiyo hivyo, hiyo habari ya Jokate bwana hamna kabisa.
Baada ya kuongea na Diamond, paparazi wetu alimtwangia simu Jokate ambapo alisikiliza madai mwanzo hadi mwisho lakini badala ya kujitetea au kufafanua, alikata simu.
WEMA ATOA LA MOYONI
Kwa upande wake, aliyekuwa mchumba wa Diamond, Wema Sepetu alipoulizwa kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa wawili hao, alisema:
Kwa upande wake, aliyekuwa mchumba wa Diamond, Wema Sepetu alipoulizwa kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa wawili hao, alisema:
“Nilisema mimi mkanipuuza, sasa mmekiona alichokifanya Jokate? Naamini ni laana yangu kwani mimi sikuwahi kumfanyia jambo lolote baya Diamond. Mungu ameona, amenilipia. Teh! Teh! Teh!
SOURCE www.freebongo.blogspot.com
Comments
Post a Comment