RIPOTI: PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MAANDAMANO YA WAZANZIBARI KATIKA HARAKATI ZA KUPINGA MUUNGANO WA TANZANIA

 Mmoja wa waandamani wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) Kisiwani Unguja,Zanzibar akionyeshan kitambaa kilicho na Damu mapema leo Asubuhi wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humo,iliyopelekea kuchomwa moto kwa moja ya makanisa pamoja baadhi ya magari yaliyokuwa yameengeshwa karibu na njia wapitazo.vurugu hizo zimeanza jana usiku baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Juimuiya hiyo.
 Waandamanaji wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) wakiendelea na maandamano yao mapema leo asubuhi.
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia Ghasia wakifanya doria katika mitaa mbali mbali ya Zanzibar mapeka leo asubuhi.
*****************
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar kwenye kisiwa cha Unguja, wameandamana kupinga muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar inayopelekea kua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Maandamano hayo yameleta mchafuko unaoendelea Zanzibar, huku ikisababisha wakazi wengi wa Unguja kujifungia majumbani mwao wakihofia usalama wao,huku biashara nyingi zikisimama pamoja na uharibifu wa mali. Polisi katika kisiwa hicho wanaendelea kufanya jitihada kutuliza ghasia hizo.
 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA