Posts

Taarifa: TFDA yafanya uchunguzi, yazitaja dawa bandia zilizopo sokoni, zitambue, jihadhari

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya bidhaa hizi.  Kati ya tarehe 28 Mei na 12 Juni 2012,  TFDA ilifanya Operesheni Maalum katika maeneo mbalimbali Kanda ya Ziwa  ikiwa ni mwendelezo wa Operesheni za kubaini bidhaa duni na bandia kwenye soko kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi nchini pamoja na Ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) za mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera. Ukaguzi na upekuzi ulifanyika kwenye maduka ya dawa, kituo cha mabasi ya kwenda mikoani, nyumba za makazi ya watu, nyumba za kulala wageni na ofisi zinazojishughulisha na kuuza shajala (stationeries). Lengo la Operesheni hii lilikuwa ni kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa duni na bandia kinyume cha Sheria ya Chakula, D

PIGA KURA YAKO SASA NIIBUKE MSHINDI KATIKA TUZO ZA BLOG

Image
Awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu kwa wadau wote wa blog hii kwa kuweza kunipigia kura za kuingia katika shindano la blog bora za kitanzania kupitia Tanzanian Blog Awards,ambapo kwa mwaka huu mchakato ulikuwa mgumu sana wa kuweza kupata blog ambazo zingeingia katika categories zilizokuwa zimewekwa kwani ni zaidi ya blog 200 zilizopendekezwa,nami nimepata bahati hiyo kupitia ninyi wadau kwa kura zenu za kutosha na kuweza kuingia katika shindano hilo. Kuanzia Jumatatu kupitia shindano la kuchagua blog bora za kitanzania inayoratibiwa na website ya http://www.tanzanianblogawards.com wadau mtaanza kupiga kura zenu kwa zile blog ambazo zimeweza kupata nafasi ya kuchaguliwa  katika vipengele tofauti tofauti , blog yako hii imepata nafasi pia ya kuingia katika shindano hili katika category ya Best Family or Personal Blog. Kura zimeanza kupigwa leo jumatatu tarehe 17th June na mwisho wa kupokea kura ni tarehe 30th June, mchakato huu utafanyika kwa muda wa wiki mbili tu kupitia

BONDIA WA URUSI AINGIA MITINI, ALIKUWA APAMBANE NA RASHID MATUMLA

Image
Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali. Wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble on the Mountain” na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini  Marekani Deidre Lorenz ambaye atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi tarehe 24 Juni mwaka huu. Deidre Lorenz anajulikana sana kwa sinema nyingi mojawapo zikiwa The Santorini Blue, Perfect Strangers, The Big Fight na nyingine nyingi. Hata hivyo Deidre Lorenz ataingia mjini Moshi akitokea nyumbani kwake New York , Marekani terehe 21 Juni tayari kikimbia mbio hizo za Mt. Kilimanjaro Marathon. Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana kama “Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia mmojawapo kuingia mitini kwa woga. Bondia Ra

WANAFUNZI WA DAR ES SALAAM, INDEPENDENT SCHOOL 2012 WAONYESHA VIPAJI VYAO

Image
Michael Kapinga akihojiwa na More Rack (kulia) baada ya kuonyesha kipaji cha hali ya juu cha kuimba,wakati wa hafla ya kujipongeza kwa kumaliza elimu ya kidaoto cha Nne na Sita iliyoandaliwa na Kampuni ya Elements Events iliyofanyika katika Ukumbi wa Litre Theatle Dar es Salaam. Michael Kapinga  akionyesha umahiri wa kuonyeshakipaji cha  kuimba wimbo wa I tried ulioimbwa na Akon na Bone Thugz, wakati wa hafla ya kujipongeza kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Dar es Salaam Independent iliyo jijini Dar es Salaam,kwa kuhitimu kidato cha Nne na cha Sita ,Hafla hiyo iliandaliwa na Saida Kapinga wa Elements Events. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam Independent iliyo jijini Dar es Salaam,Owen Karonga na Carine Maro ambao waliibuka washindi kwaa kuwanadhifu katika hafla ya kujipongeza kwa kumaliza elimu ya kidaoto cha Nne na cha sita iliyofanyika katika Ukumbi wa Litre Theatle Oysterbay ,Kulia ni Mkurugenzi wa Elements Eve

EXCLUSIVE: WAREMBO WAKIJIANDAA NA MISS REDD’S WORLD TANZANIA

Image
    source www.freebongo.blogspot.com

PICHA NA MAJINA YA WALIOPATA TUZO ZA TASWA

Image
MAJINA YA WASHINDI WA TUZO ZA TASWA: 1: OLIMPIKI MAALUM-Zanzibar Ahmada Bakar: 2:OLIMPIKI MAALUM-TANZANIA BARA HERITH SULEIMAN 3: PARALIMPIKI: WANAUME ZAHARANI MWENEMTI 4:PARALIMPIKI: WANAWAKE FAUDHIA CHAFUMBWE 5: KIKAPU: WANAUME GEORGE TARIMO: 6: KIKAPU WANAWAKE EVODIA KAZINJA:- 7: NETIBOLI: LILIAN SYLIDION 8: GOFU WANAWAKE: MADINA IDDI 9: GOFU WANAUME: Frank Roman: 10: NGUMI ZA RIDHAA SULEIMAN SALUM KIDUNDA 12: WAOGELEAJI MWANAMKE MAGDALENA MOSHI WAOGELEAJI MWANAUME AMMAAR GHADIYALI – MEN 13:JUDO… AZZAN HUSSEIN KHAMIS (ZANZIBAR) 14:JUDO BARA: . MBAROUK SELEMANI 14: WAVU WANAWAKE THERESIA ABWAO 15: WAVU WANAUME MBWANA ALLY 16: NGUMI ZA KULIPWA Nasibu Ramadhan 17. TENISI:Wanaume WAZIRI SALUMU 18. TENISI WANAWAKE: REHEMA ATHUMANI 20: BAISKELI (Wanawake) Sophia Hussein - 21: BAISKELI WANAUME Richard Laizer 22: WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE Mbwana Samatta- 23: MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI SHOMARI KAPOMBE- (so

P SQUARE WASITISHA MAWASILIANO KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

Image
Kundi la wasanii mapacha wa Nigeria P-Square limesema kwa sasa halitumii kabisa mtandao wa Facebook kama njia ya kuwasiliana. Jana kupitia Twitter, kundi hilo limetweet meseji kadhaa kuhusu kuwaonya mashabiki na watu wengine kuhusu watu wanaotumia majina yao kutapeli watu. “We no longer communicate via FACEBOOK pls tell a friend.. Thanks,” aliandika Peter Okoye ambaye mara nyingi ni muongeaji zaidi kuliko Paul. “I and @rudeboypsquare and @JUDEENGEES no longer communicate via FACEBOOK pls beware of FRAUDSTARS.” Pia waliambatanisha picha ya chat ya Facebook inayoonesha kuwa mazungumzo yalikuwa yakifanywa na kaka yao Jude Okoye. Katika hatua nyingine mpaka asubuhi ya ijumaa , video ya wimbo wao mpya uitwao ‘Beautiful Onyenye’ waliomshirikisha Rick Ross imeangaliwa mara 646,248 siku tatu tu baada ya kuwekwa YouTube.

AVRIL KUICHOKOZA BONGO MWEZI UJAO

Image
Songstress wa " Chokoza" ambaye yuko chini ya label ya Ogopa Deejays all the way from area coded 254 atatua bongo next month.  Infoz za uhakika toka kwa Linex ambaye kwa sasa anazi-top  radio airwaves kwa ngoma yake ya "Alifora" ,  amesema kwamba Avril ambaye jina lake kamili ni Judith Nyambura Mwangi mwezi ujao atadondoka nchini kwa ajili ya kuja kupamba uzinduzi wa video ya wimbo wa "Aifora Aifora" bila kusahau album yake ya " Moyo wa Subira" .   "Kila kitu kiko onset, mwanadashosti hana tatizo na mtu kinachosubiriwa ni siku ufike atokelezee kuwasha moto at Maisha Club tarehe saba ya mwezi ujao" - Linex ambaye pia ni msanii wa ngoma za "Mama Halima" na " Moyo wa Subira".   Kama ulikuwa hujui Avril ambaye ngoma yake ya kwanza kwenye game ilikuwa "Mama" kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi anakosoma interior design

TANZANIAN BLOGS AWARDS HIYO NAMI NIMO...SO JIANDAENI WADAU KUNIPIGIA KURA ZENU

Image
Awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu kwa wadau wote wa blog hii kwa kuweza kunipigia kura za kuingia katika shindano la blog bora za kitanzania kupitia Tanzanian Blog Awards,ambapo kwa mwaka huu mchakato ulikuwa mgumu sana wa kuweza kupata blog ambazo zingeingia katika categories zilizokuwa zimewekwa kwani ni zaidi ya blog 200 zilizopendekezwa,nami nimepata bahati hiyo kupitia ninyi wadau kwa kura zenu za kutosha na kuweza kuingia katika shindano hilo. Kuanzia Jumatatu kupitia shindano la kuchagua blog bora za kitanzania inayoratibiwa na website ya http://www.tanzanianblogawards.com wadau mtaanza kupiga kura zenu kwa zile blog ambazo zimeweza kupata nafasi ya kuchaguliwa  katika vipengele tofauti tofauti , blog yako hii imepata nafasi pia ya kuingia katika shindano hili katika category ya Best Family or Personal Blog. Kura zitaanza kupigwa kuanzia  jumatatu  tarehe 17th June na mwisho wa kupoke kura ni tarehe 30th June, mchakato huu utafanyika kwa muda wa wiki mbili tu k

“PARTY ZONE”-AY Ft. MARCO CHALI(OFFICIAL VIDEO)

Image
Hatimaye video ya wimbo Party Zone kutoka kwa AY akiwa amemshirikisha Marco Chali (producer ambaye siku hizi anaanza kuja juu kwa utundu mwingine ndani ya muziki) imetoka. Inasemekana kuwa mojawapo ya video za gharama kubwa kabisa zilizowahi kufanyika miongoni mwa wasanii wetu. Hii hapa chini;

PREZZO KUJITOA BIG BROTHER?

Image
. Ishu ambayo imewashangaza wengi ni pale ambapo mwakilishi wa Kenya kwenye jumba la Big Brother CMB Prezzo kutangaza kwamba amechoka maisha ya kuishi kama mfungwa kwenye jumba hilo.   Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kwamba hii ishu imetokea wakati Big Brother alipotangaza kupiga marufuku pombe kwa washiriki ndani ya jumba hilo, Prezzo alishikwa hasira na kusema kwamba anaweza kuondoka muda wowote, na anahisi wakati umefika. Prezzo alimaind mpaka akawa anabishana na washiriki wenzake akiwemo Keita na kutaka mlango ufunguliwe aondoke lakini baadhi ya washiriki wenzake walimsihi asifanye hivyo.   Huu mchongo umetokea siku 30 baada ya Prezzo kuwa trending topic kwa wakenya kutokana na kuchaguliwa kwake kwenda big brother ambapo wengi walikua wanamdiss kwamba haikutakiwa apelekwe BBA ambapo Nakumbuka Naziz wa Necessary Noise ambae ni mshkaji wa Prezzo siku 31 zilizopita Alisema kwamba wengi wamemkosoa lakini ni kwa sababu hawamjui

BET AWARDS 2012: Camp Mulla Waomba Kura za wana Afrika Mashariki

Image
Zikiwa zimesalia siku 16 tu kabla ya kufanyika kwa tuzo za BET mwaka 2012, kundi la vijana watano kutoka Kenya, Campmulla limewaomba wapenzi wa muziki wa Afrika Mashariki kuwapigia kura. Kundi hilo limetajwa kuwania kipengele cha Best International Act Afrika likishindana na wasanii kama Ice Prince, WizKid wa Nigeria, Sarkodie wa Ghana, Lira wa Afrika Kusini na Makobe wa Mali.  Ni mara ya kwanza kwa msanii ama kundi la Afrika Mashariki kutajwa kwenye tuzo hizo. Tuzo za BET zitatolelwa July 1, na host atakuwa muigizaji mkongwe wa filamu Samuel L Jackson. Leo kundi hilo kupitia Facebook limeandika, “ Support the Camp Mulla Movement and keep sharing; http://www.bet.com/topics/c/camp-mulla.html.” Wasanii watakaotumbuiza mwaka huu ni pamoja na Usher, Chris Brown, Nicki Minaj, Big Sean na 2 Chainz