BONDIA WA URUSI AINGIA MITINI, ALIKUWA APAMBANE NA RASHID MATUMLA
Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni
kali. Wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble
on the Mountain” na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka
nchini Marekani Deidre Lorenz ambaye
atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi tarehe 24
Juni mwaka huu.
Deidre Lorenz anajulikana sana kwa sinema nyingi mojawapo
zikiwa The Santorini Blue, Perfect
Strangers, The Big Fight na nyingine nyingi. Hata hivyo Deidre Lorenz
ataingia mjini Moshi akitokea nyumbani kwake New York , Marekani terehe 21 Juni
tayari kikimbia mbio hizo za Mt. Kilimanjaro Marathon.
Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana kama
“Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya
shirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara ya kwanza kwa
mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia
mmojawapo kuingia mitini kwa woga.
Bondia Rashid Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana
rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.
Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na
Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani
(WBU). Akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa
ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali
ya juu.
Hata hivyo Rashid Matumla
amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi
huyo!
source www.fullshangweblog.com
Comments
Post a Comment