P SQUARE WASITISHA MAWASILIANO KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK
Kundi la wasanii mapacha wa Nigeria P-Square limesema kwa sasa halitumii kabisa mtandao wa Facebook kama njia ya kuwasiliana.
Jana kupitia Twitter, kundi hilo limetweet meseji kadhaa kuhusu kuwaonya mashabiki na watu wengine kuhusu watu wanaotumia majina yao kutapeli watu.
“We no longer communicate via FACEBOOK pls tell a friend.. Thanks,” aliandika Peter Okoye ambaye mara nyingi ni muongeaji zaidi kuliko Paul.
“I and @rudeboypsquare and @JUDEENGEES no longer communicate via FACEBOOK pls beware of FRAUDSTARS.”
Pia waliambatanisha picha ya chat ya Facebook inayoonesha kuwa mazungumzo yalikuwa yakifanywa na kaka yao Jude Okoye.
Katika hatua nyingine mpaka asubuhi ya ijumaa , video ya wimbo wao mpya uitwao ‘Beautiful Onyenye’ waliomshirikisha Rick Ross imeangaliwa mara 646,248 siku tatu tu baada ya kuwekwa YouTube.
Comments
Post a Comment