AVRIL KUICHOKOZA BONGO MWEZI UJAO


Songstress wa "Chokoza" ambaye yuko chini ya label ya Ogopa Deejays all the way from area coded 254 atatua bongo next month.

 Infoz za uhakika toka kwa Linex ambaye kwa sasa anazi-top  radio airwaves kwa ngoma yake ya "Alifora",  amesema kwamba Avril ambaye jina lake kamili ni Judith Nyambura Mwangi mwezi ujao atadondoka nchini kwa ajili ya kuja kupamba uzinduzi wa video ya wimbo wa "Aifora Aifora" bila kusahau album yake ya "Moyo wa Subira".

 "Kila kitu kiko onset, mwanadashosti hana tatizo na mtu kinachosubiriwa ni siku ufike atokelezee kuwasha moto at Maisha Club tarehe saba ya mwezi ujao" - Linex ambaye pia ni msanii wa ngoma za "Mama Halima" na "Moyo wa Subira".
 
Kama ulikuwa hujui Avril ambaye ngoma yake ya kwanza kwenye game ilikuwa "Mama" kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi anakosoma interior design

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA