TANZANIAN BLOGS AWARDS HIYO NAMI NIMO...SO JIANDAENI WADAU KUNIPIGIA KURA ZENU
Awali ya yote napenda kutoa shukurani zangu kwa wadau wote wa blog hii kwa kuweza kunipigia kura za kuingia katika shindano la blog bora za kitanzania kupitia Tanzanian Blog Awards,ambapo kwa mwaka huu mchakato ulikuwa mgumu sana wa kuweza kupata blog ambazo zingeingia katika categories zilizokuwa zimewekwa kwani ni zaidi ya blog 200 zilizopendekezwa,nami nimepata bahati hiyo kupitia ninyi wadau kwa kura zenu za kutosha na kuweza kuingia katika shindano hilo.
Kuanzia Jumatatu kupitia shindano la kuchagua blog bora za kitanzania inayoratibiwa na website ya http://www.tanzanianblogawards.com wadau mtaanza kupiga kura zenu kwa zile blog ambazo zimeweza kupata nafasi ya kuchaguliwa katika vipengele tofauti tofauti , blog yako hii imepata nafasi pia ya kuingia katika shindano hili katika category ya Best Family
or Personal Blog. Kura zitaanza kupigwa kuanzia jumatatu tarehe 17th June na mwisho wa kupoke kura ni tarehe 30th June, mchakato huu utafanyika kwa muda wa wiki mbili tu kupitia blog ya tanzanianblogawards.
Mungu awabariki sana
Comments
Post a Comment