WAHAMIAJI 42 WAFA DODOMA
WAHAMIAJI haramu 42 raia wa Ethiopia wamekufa katika Kijiji cha Chitego Tarafa ya Zoisa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakiwa safarini kutoka Ethiopia kwenda Malawi. Kamanda Zelothe Stephen Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wengine 74 hali zao ni mbaya sana kutokana na kukosa chakula na maji hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu. Baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wahamiaji hao waligunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakienda katika shughuli zao za kilimo jana asubuhi. Taarifa hiyo inadai kuwa wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa hoi usiku wa kuamkia leo (jana)baada ya kushushwa katika lori ambalo bodi lake ni la Kontena Taarifa hizo za awali zinasema kuwa wahamiaji hao walikuwa 116 ambao walikuwa wamefungiwa katika kontena hilo na hivyo kukosa hewa kutokana na kulundikana. Mpaka sasa haijulikani gari hilo lina milikiwa na nani kwani wahamaji walionusulika wengi wapo katika hali mbaya. Mpaka sasa hak