WAHAMIAJI 42 WAFA DODOMA

WAHAMIAJI haramu 42 raia wa Ethiopia wamekufa katika Kijiji cha Chitego Tarafa ya Zoisa Wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakiwa safarini kutoka Ethiopia kwenda Malawi.
Kamanda Zelothe Stephen
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa wengine 74 hali zao ni mbaya sana kutokana na kukosa chakula na maji hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu.

Baadhi ya mashuhuda ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wahamiaji hao waligunduliwa na wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wakienda katika shughuli zao za kilimo jana asubuhi.

Taarifa hiyo inadai kuwa wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa hoi usiku wa kuamkia leo (jana)baada ya kushushwa katika lori ambalo bodi lake ni la Kontena

Taarifa hizo za awali zinasema kuwa wahamiaji hao walikuwa 116 ambao walikuwa wamefungiwa katika kontena hilo na hivyo kukosa hewa kutokana na kulundikana.

 Mpaka sasa haijulikani gari hilo lina milikiwa na nani kwani wahamaji walionusulika wengi wapo katika hali mbaya.

 Mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku wahamaji watano wanaendelea kupata matibabu katika Zahanati ya kijiji cha Chitego ambapo wengine waliobaki wamehifadhiwa katika kanisa la Anglikan wakipatiwa huduma mbalimbali.
 

Huduma hizo mbalimbali ni pamoja na kupewa maji , uji na matibabu.

 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuhaidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA