Posts

Usalama Kuimarishwa Mkoani Mara Wakati wa Zoezi la Sensa

Na Boniphace Mgendi SERIKALI mkoani Mara,imeviagiza vyombo vya dola na viongozi mbalimbali wa ngazi zote mkoani humo,kuhakikisha wanasimamia hali ya usalama kwa kuwachukulia hatua kali watu wote ambao wataonekana kukwamisha mafanikio ya zoezi la Sensa ya watu na makazi,ambalo linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu.   Kauli hiyo ilitolewa mjini Musoma na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabiriel Tupa wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya wakufunzi wa Sensa ya watu na makazi ngazi ya mkoa.   Amesema serikali haitakubali baadhi ya watu kuwa chanzo cha kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa taifa na ambalo linatarajia kiasi kikubwa cha fedha,ambapo amesema ni wajibu wa kila kiongozi kufanya uhamasishaji kwaajili ya kuwezesha mafanikio katika zoezi hilo. Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alitumia nafasi hiyo kuonya kwamba kamwe serikali hatasita kuchukua hatua kw

PUBLISH YOUR ARTICLE HERE

DO YOU HAVE AN ARTICLE?DO YOU WANT TO PUBLISH YOUR ARTICLE?DO YOU FIND THE BLOG THAT YOU CAN PUBLISH IT?THIS IS YOUR RIGHT CHOICE TO ACCOMPLISH YOUR TASK,SEND  YOUR ARTICLE TO MY EMAIL ADDRESS  kelvinnyanja@yahoo.com or kelvinnyanja@gmail.com  AND I WILL PUBLISH IT FREE OF CHARGE ,           HAVE A LOVELY WEEKEND GUYZ

HAPPY BIRTHDAY MA BRO JAILESI

Image
WISH ALL DA BEST IN YOUR LIFE,ENJOY THIS BEAUTIFUL DAY BRO.

KUMBE ABIRIA NAO WANAPENDA NJIA ZA SHORTCUT

Juzi nilikuwa natoka Shinyanga katika miangaiko ya hapa na pale,nilikuwa nimepanda basi la AM linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Tabora na Mwanza,mimi nilipandia shinyanga kurudi Mwanza,sasa kilichonishangaza ni kwamba serikali inajitahidi kuboresha barabara zetu ili magari yaweze kupita katika barabara za lami lakini bado kuna madereva wengine hawazitumii barabara hizo na kufanya wao wanavyojua. Tulipita katika barabara ya (Old Shinyanga Road) barabara ambayo haina lami lakini pia kuna vumbi sana kiasi kwamba mwili wote ulikuwa umeogeshwa kwa vumbi la barabara hiyo,nilijaribu kuwadadisi abiria wenzangu hivi ni kwa nini dereva hatumii barabara ya lami anapita huku kwenye barabara isiyokuwa na kiwango walinijibu kuwa "Njia hii ni shortcut kuliko tukitumia barabara ya lami" nikajaribu kujiuliza maswali hivi hata abiria wao wenyewe wanapenda mambo ya shotcut na wako satisfied kabisa na jambo hili,kama mdau wa bolg hii mawazo yako ni yapi kuhusiano na jambo hili??????

17 MARA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA MOROGORO

Na Shomari Binda, Timu ya soka ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Mkoa wa Mara leo imeahidi kuitoka timu ya vijana ya Mkoa wa Morogoro katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali kwenye uwanja wa karume jijini Dar es salam. Akizungumza kwa njia ya simu na BINDA NEWS kutoka jijini humo,Meneja wa vijana wa Mara Sindbad Madenge amesema kikosi cha vijana wake wapo katika hali nzuri katika kuingia katika mchezo huo na kudai kuwa kikosi chao hakina majeruhi yeyote na wapo tayari kwa mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni. Alisema kuwa kitendo cha kuwaondosha katika michuano hiyo mabingwa watetezi timu ya mkoa wa Kigoma kimewaongzea hali wachezaji wake lakini amewataka kutobweteka na matokeo ya mchezo huo katika hatua ya 16 bora. Katika hatua nyingine Madenge ametuma salama za rambirambi kufuatia kifo cha mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoani Mara Fabian Samo kilichotokea Julai 10 na kuiomba familia yake pamoja na wadau wote wa michezo Mkoa

POLENI KWA USUMBUFU

Poleni sana kwa usumbufu uliojitokeza kwa kipindi chote kwa wale wapenzi wa blog hii ,nilikuwa katika kipindi cha mitihani hivyo nilikuwa sipati kabisa muda wa kutosha kuweza ku uptodate information za kutosha,lakini hivi sasa msijali tena nimesharudi so more information zitakuwepo za kutosha.Pia nawashukuru sana na sana kwa kuweza kunipigia kura za kutosha mpaka kuweza kuibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha blog bora za kitanzania kwangu ni heshima kubwa sana lakini pia ni heshima kwa wapenzi wote wa blog hii kwa kuwa wamefanya chaguo halisi. Nawatakia kazi njema za kulijenga Taifa.

THE WINNER......

Image

OMMY DIMPOZ NA DJ ALLY WASHIRIKI PARTY YA KUZINDUA STONE CLUB MPYaaaaaaaa.

Image
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz usiku wa kuamkia leo (nikimaanisha jana alhamisi) ameshiriki vyema kwenye party ya kuzindua Stone Club ambayo imekuja kivingine, na sevis mpya na wahudumu wapya  mara baada ya ukarabati wa muda mrefu.  Party hiyo iliyokuwa ya kimya kimya ilinogeshwa na dance la nguvu lililomwagwa na Ommy Dimpoz akishirikiana na densaz wake mahiri. Dance likiendelea katika stage ndani ya party hilo ambapo usiku huo pia ulitumika kama usiku wa kwanza mara baada ya wanavyuo kumaliza pepa. On the one and Two alisimama Dj Ally ' mzee wa kitu juu ya kitu' toka A- town ambaye alifanya makamuzi ya hatari uspime ndani ya Stone Club Mpyaaa iliyofungwa sound full kiwango ..... Dj Ally amesaini 'kontrakti'  ya muda wa kutosha hivyo ataendelea kukisanukisha hapa. Ommy Dimpoz kwa poz akicheza na shabiki wake mara baada ya mzuka kumpanda...

VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO J3

Image
. . . . . . . . . . . . . .

FAINALI EURO 2012 , SPAIN 4 – ITALY 0

Image
Fernando Torres, Juan Mata, Silva na Alba ndio wameandika hizo nne za Hispania. . . . . .

WAZIRI MKUU AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA KITAIFA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Image
 Wazi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikabidhi zawadi ya cheti mshindi wa kwanza wa jiji lililofanya vizuri kwenye maonyesho hayo kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.  Waziri mkuu mh. Pinda akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ndikilo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho hayo toka halmashauri mbalimbali nchini zilizoshiriki.  Watumishi wa ofisi ya TAMISEMI wakiwa kwenye banda la maonyesho la ofisi hiyo katika viwanja vya CCM Kirumba wakisubiri kutoa maelezo kwa waziri mkuu ambaye alipita kutembelea mabanda ya maonyesho.  Picha ya mchoro wa Jengola kisasa la kliniki ya wajawazito na watoto lililokwisha anza ujenzi wake katika eneo la mtaa wa Utemini jijini Mwanza ambalo likikamilika ujenzi wake litakuwa na taswira hii. Jengo hili litakuwa mbadala wa jengo ambalo linatarajiwa kuvunjwa la Kliniki ya zamani  lililopo mtaa wa barabara ya Makongoro. kupisha ujenzi wa jengo la Benki kuu ya Ta

ASANTENI WADAU KWA KUNIPA USHINDI

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo linatokea katika maisha yangu kila kukicha,pia na kuwashukuru Ndugu,jamaa na marafiki walioko katika mtandao wa facebook kwa kuweza kunipigia kura za kutosha na kuweza kufanikisha kuibuka mshindi katika shindano la kutafuta blog bora za kitanzania ambalo limefanyika zaidi ya miezi 2 katika kupata washindi. Shindano hili linaratibiwa na website ya www.tanzanianblogawards.com ambayo ilianzishwa mwaka jana na mwaka huu shindano  limefanyika kwa mara ya pili likiwa na nia ya kuweza kutangaza blogs mbalimbali ambazo zinamilikiwa na watanzania waliopo nchini na wale waishio ng'ambo lakini pia kuweza kuwathamini kwa kile wanachokifanya katika kuhabarisha jamii kwaa ujumla. Shindano ili lilianza miezi 2 iliyopita kwanza kwa kuweza kunominate blog ambayo inafaa kuingia katika category mbalimbali ambazo zilikuwa zimeanishwa na waratibu,kwa mwaka huu zaidi ya blog 600 za kitanzania zilipendekezwa kuingia katika shindano hili na