By kijungu jiko HIZI NDIZO HOJA ZA MPOTOSHAJI JUU YA UTENDAJI WA SERIKALI YA WANAFUNZI SAUTSO. MAJIBU YAKE YAPO CHINI. M alisa Godlisten Rais wa Serikali ya Wanafunzi SAUTSO Chuo kikuu cha St Augustine umetudharirisha mpaka tunaona aibu sasa na vuguvugu la CHADEMA , tena tuliingia kwa mbwembwe kali kuwa tutakuwa wakombozi wa watu, waliotuchagua kwa kura nyingi richa ya kuwepo nguvu kubwa ya viongozi waliotangulia hasa Rais Bwana Cosmas Mataba na Anna Mushi, Spika wa Bunge Bw Maro Pius, na aliyekuwa Waziri mkuu Bw Leonard Mafuru, tukamchagua kijana huyu aliedaiwa machachari akitokea Baraza la vijana la CHADEMA yani BAVICHA kwa kishindo cha zaidi ya asilimia 75% licha ya hira za Mataba na Tume yake ya Uchaguzi, tukashinda uchaguzi kwa mbwembwe kabisa tukimtupilia mbali mgombea aliefadhiriwa kwa gharama kubwa na CCM Bwana Antony na Mgombea mwenza Bibie Alice, tuliingia huku wanafunzi wakiwa na matumaini makubwa ya kuona mabadiriko kufuatia manung’uniko ya serikari ilio tangulia ya