GODLISTEN MALISA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI AJIBU HOJA POTOFU ZILIZOSAMBAZWA MTANDAONI NA WAPOTOSHAJI JUU YA UTENDAJI WA SERIKALI YAKE.

By kijungu jiko
HIZI NDIZO HOJA ZA MPOTOSHAJI JUU YA UTENDAJI WA SERIKALI YA WANAFUNZI SAUTSO. MAJIBU YAKE YAPO CHINI.

Malisa Godlisten Rais wa Serikali ya Wanafunzi SAUTSO Chuo kikuu cha St Augustine umetudharirisha mpaka tunaona aibu sasa na vuguvugu la CHADEMA, tena tuliingia kwa mbwembwe kali kuwa tutakuwa wakombozi wa watu, waliotuchagua kwa kura nyingi richa ya kuwepo nguvu kubwa ya viongozi waliotangulia hasa Rais Bwana Cosmas Mataba na Anna Mushi, Spika wa Bunge Bw Maro Pius, na aliyekuwa Waziri mkuu Bw Leonard Mafuru, tukamchagua kijana huyu aliedaiwa machachari akitokea Baraza la vijana la CHADEMA yani BAVICHA kwa kishindo cha zaidi ya asilimia 75% licha ya hira za Mataba na Tume yake ya Uchaguzi, tukashinda uchaguzi kwa mbwembwe kabisa tukimtupilia mbali mgombea aliefadhiriwa kwa gharama kubwa na CCM Bwana Antony na Mgombea mwenza Bibie Alice, tuliingia huku wanafunzi wakiwa na matumaini makubwa ya kuona mabadiriko kufuatia manung’uniko ya serikari ilio tangulia ya Bwana Mataba, Maro na Mafuru kutuhumiwa kwa ufisadi, ubadhirifu Ngono na matumizi mabaya ya ofisi na kupeana madaraka ya SAUTSO (Maro na Mataba wanadaiwa kuongoza serikali hiyo ya 2011/2012 kwa ubia wa makubaliano maalum…. Source kinasa sauti cha siri kilichomrekodi Bwana Maro kwa siri na vijana wa CHADEMA nyumbani kwake Nganza). Tuliingia tukiwalaumu wenzetu waliotutangulia lakini kwa mtazamo wa haraka hakika wao na sisi wana unafuu mkubwa wa kukumbukwa, hakuna kilichofanyika wala kubadilika, Ahadi zote tulizo ahidi mpaka wakati huu tunapoelekea kufanya uchaguzi tena hakuna dalili kuwa tutafanya chochote,


Tumeshindwa kabisa kutekeleza ahadi zifuatazo:-
1. Tuliahidi kujenga kutuo cha polisi katika jamii hii ya watu zaidi ya 26,000 ili kupambana na vitendo vya ubakaji wa dada zetu katika maeneo tofauti ya vuinga vya chuo hiki tumeshindwa.

2. Tuliahidi kuhamia kwenye ofisi mpya za SAUTSO ili kuongeza ufanisi wa shughuri zetu mpaka sasa hivi haifahamiki mradi huo umeishia wapi.

3. Tuliahidi kupambana na matatizo ya mikopo kwa wanafunzi lakini hakika hivi sasa tuna matatizo makubwa katika idara ya mikopo kuliko hata wakati wa Mataba, mikopo inachelewa, majina yanachanganyika, na mpaka hivi sasa kuna watu hawajaona mkopo since waje mwezi September.

4. Tuliahidi kuanzisha utaratibu wa kutunza kumbukumbu za kudumu lakini hilo limeshindikana.

5. Tuliahidi kurekebisha miundo mbinu ambayo sio rafiki kwa wenzetu wenye changamoto ya viungo sijui tumeishia wapi.

6. Bunge limekuwa genge la malumbano, migawanyiko, makundi ya urais ujao, na mijadara ya miradi isiyotekelezeka,

7. Umeme madarasani bado na viongeza sauti bado ni kero.
8. Unyanyasaji wa kimapenzi umekithiri hasa kwa viongozi wa kike pale SAUTSO.

9. Kuna serikali ya siri ya Bw Tungaraza ndani ya serikali ya Bw Malisa,
10. Migawanyiko iliyotokana na maslahi binafsi na uroho wa fedha umezidi.

11. Ubadhirifu wa pesa umeongezeka na pesa zinaishia kwenye mikono ya mabosi wachache wa SAUTSO.

12. Bwana Malisa mwenyewe anaongoza kwa matumizi mabaya ya fedha za wanafunzi, amesafiri zaidi kwa Ndege hata zaidi ya Bwana Mataba na Serikali yake, hakai ofisini, hatekelezi majukumu ya SAUTSO kwa wakati, wanafuzi wanalaumu kuwa muda mwingi
 pamefungwa, na wasaidizi wake wana kauri mbaya hasa idara ya mikopo, Malisa yuko busy facebook mara sijui naenda Lunch, nimepoteza simu, mara sijui najiandaa kupanda ndege, mara sijui natoka wapi naenda wapi je hiyo ndio spirit ya wana BAVICHA.

13. Tuliahidi Basi la SAUTSO mradi umeishia hewani bila maelezo.

14. Funga kazi ni kitendo cha aibu cha maandalizi ya michezo ya Vyuo vya SAUT kule Morogoro hali ilikuwa ni ya aibu, michezo mibovu, hakukuwa na motisha, zawadi hovyo, ugomvi, mazingira magumu, nilibahatika kupata taarifa kuhusu michezo ya aina hiyo ambayo ilifanyika Mtwara wakati wa Bw Mataba, yani ni mara Elfu kumi Tamasha la Mtwara, kulikuwa na msisimko, watu wengi, zawadi nzuri, malazi safi, chakula kingi, matibabu, michezo mingi, na Ratiba ya kueleweka, yani kilichofanyika Morogoro hakikuwa tofauti na Kombe la mbuzi kwenye shule Fulani za kata.

15. Chini ya Uongozi wa Malisa na wenzake Umoja wa vyuo vya SAUT Umekuwa na picha mbaya, pesa zilitafunwa, watu wakapigana, zawadi zikaibiwa, makombe yakachanganyikana, mgeni rasmi kwa aibu kubwa akapigwa na maganda ya ndizi, mayai viza na kondomu zilizotumika ebu pata picha hali ingekuwa nihiyo kule Mtwara ambapo mgeni rasmi alikuwa ni VC KITIMA mwenyewe na wakuu wengine wa SAUT Tanzania nzima.

Aliyetuponza mpaka hapa ni mambo ni mengi ila TUNGARAZA ametuponza pia kwa kujaribu kuingilia kwa siri kila jambo, Vijana wa BAVICHA tuliohusika katika harakati za kukuweka madarakani tumeishiwa na imani kabisa tunahitaji mabadiriko ya vijana wajao katika nafasi hizi tulijitoa kwa moyo na maisha yetu mpaka hata kufikia hatua ya kuweka masomo yetu hatarini kwa kupambana na viongozi waliotangulia Bw Mataba na wenzie kufanikisha hili ila tumekatishwa tamaa.


 GODLISTEN MALISA AKIJIBU HOJA POTOFU ZILIZOTOLEWA HAPO JUU ZA KUICHAFUA SERIKALI YAKE.

HUU NDIO UKWELI KUHUSU KAMANDA MALISA NA CHADEMA
Katika siku za hivi karibuni kumetokea kundi la wanaCCM ambao wamekuwa wakijiita wanaCHADEMA na kutoa matamko ya kukitukana chama na viongozi wake. Vuguvugu hili lilianzia kwa watu waliojiita viongozi wa BAVICHA na kuanza kumshambulia Dr.Slaa, wakaenda kwa Mbowe. Wakatengeneza makundi ndani ya chama, lakini hatimaye kamati kuu ikawabaini wale vigogo na kuwatimua.

Lakini kwa kuwa ulikuwa mtandao wapo wanaoendelea na kazi yao ya kujaribu kubomoa chama, huku wengine wakijiita makamanda. Sasa wamehamia BAVICHA na matawi ya chama katika vyuo vikuu wakijaribu kupotosha. Ijumaa ya tar.12/01/2013 mmojawao akapost thread hapa JF inayojaribu kudiscredit Chadema tawi la chuo kikuu cha SAUT Mwanza na uongozi mzima wa serikali ya chuo hicho inayoongozwa na kamanda Malisa aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama.

Nimelazimika kujibu tuhuma hizo za majungu baada ya kuona kuna upotoshaji wa hali ya juu na tuhuma ambazo hazina vidhibitisho ndani yake (facts). Nasema taarifa iliyotolewa ni upotoshaji maana mimi nimebahatika kufanya kazi katika serikali zote mbili. Ile ya Mataba (CCM) na hii ya Malisa (CHADEMA). Wakati wa Mataba nilikuwa kiongozi na hiii ya Malisa ni kiongozi pia japo katika wizara tofauti. Hivyo naamini naweza kutoa mlinganyo sahihi kuliko mtu aliyekuwa nje ya system so anaongea majungu ili kufanikisha matakwa binafsi.

Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa kwa Malisa na serikali yake ni kushindwa kujenga kituo cha Polisi. Ukweli ni kwamba Malisa hakuahidi kujenga kituo cha Polisi. Ila aliahidi kuimarisha hali ya usalama kwa wanafunzi kwa kushirikiana na uongozi wa chuo. Kwenye Ilani yake ya uchaguzi ameandika “….In collaboration with University management we shall make sure we maintain peace and security among SAUT students. Ensuring the Police patrol for Off-Campus hostels and if the situation will continue to be worse I will ask for police station….”

Mtu yeyote mwenye nakala ya manifesto ya Malisa anaweza kudhibitisha maneno haya. Sasa kwa uelewa wangu mdogo wa kiingereza sijaona mahali Malisa alipoahidi kujenga kituo cha Polisi. Kama sijakosea nadhani alimaanisha kutafuta patrol ya polisi kwa hostel za nje na kama hali ikiendelea kuwa mbaya ataomba kujengwa kituo cha Polisi. Nadhani sentensi ya pili ina maana sana katika kuleta tafsiri sahihi. Malisa anasema kama hali ikiendelea kuwa mbaya, ataomba kituo cha polisi. Hali ipi? Na je hiyo hali imeendelea kuwa mbaya kama alivyoeleza?

Ikumbukwe wakati Malisa anaingia ofisini vitendo vya kihalifu vilikuwa vimeshamiri. Wanafunzi walikuwa wanavamiwa hostel, wanapigwa na kuporwa mali zao. Lakini vibaka nao walikuwa wakikamatwa na kuuawa. Kwa kipindi cha mwezi April peke yake waliuawa majambazi wanne, watatu kwa kuchomwa moto na mmoja kupigwa mawe na wanafunzi. Ukajengeka uadui mkubwa kati ya wanafunzi na wakazi wa maeneo jirani na chuo. Kwa kweli hali ilikuwa mbaya.

Je hali imeendele kuwa mbaya? Tangu Malisa ameingia ofisini mwaka jana hakuna matukio ya kutisha kama ilivyokua awali. Majambazi kuvamia hostel kwa silaha za moto hakuna tena. Je Malisa amefanya nini? Amehakikisha Patrol ya polisi inakuwepo kila siku kwa ajili ya kufanya doria maeneo ya chuo. Katika siku za awali Polisi walikuwa hawafiki kila siku kutokana na changamoto ya gari. Wakidai kuwa gari lao linatumika pia katika shughuli nyingine. Lakini mwezi June mwaka 2012 Makamu Mkuu wa Chuo akaitisha kikao na OCD wa Nyamagana na Rais Malisa. Hatimaye wakakubaliana gari aina ya Land Cruser mali ya chuo litumike kufanya Patrol. Tangu wakati huo gari hilo limekuwa likifanya Patrol hadi leo na limesaidia sana kupunguza vitendo vya kihalifu. Namba za simu za gari zipo nje ya ofisi ya SAUTSO kwa yeyote mwenye kuhitaji msaada huo. Sasa kwa initiatives hizi, hoja ya Malisa kushindwa kujenga kituo cha polisi inatoka wapi kama si majungu?


Lakini kwa waliokuwepo siku ya kufungua chuo Malisa alihutubia mbele ya uongozi wa chuo na miongoni mwa mambo aliyoeleza ni hilo linalodaiwa la kituo cha polisi. Alisema amepokea nakala ya barua kutoka kwa RPC ikiwa imeambatana na ramani ya ujenzi, ikielekeza kuwa jeshi la polisi limejipanga kujenga kituo cha Polisi kijiji cha Luchelele nje kidogo ya chuo. Nakala ya barua hiyo ipo pia kwa Makamu Mkuu wa chuo na Dean of students. Lakini ikumbukwe Jeshi la Polisi halijaamua tu kujenga kituo hicho from no where. Kuna haja ya kuamini kuwa Malisa amefanya kazi ya ziada kushawishi mpango huo.

Waliokuwepo kwenye kikao kati ya aliyekuwa Meya wa jiji Mh.Manyerere na serikali ya wanafunzi, mwezi August mwaka jana walimsikia jinsi alivyosifia juhudi za serikali ya wanafunzi kudai Police Station. Sasa anapoibuka mtu na kudai Malisa kashindwa kujenga kituo cha polisi ana maana gani kama sio majungu? Walitegemea Malisa kutoa fedha zake mfukoni na kujenga kituo? Ni vizuri watu hao wakaweza kutofautisha Kituo cha Polisi na Kibanda cha M-Pesa. Kibanda cha M-PESA unaweza kujenga hata kwa siku moja. Lakini kituo cha polisi kina taratibu zake za kisheria na kiusalama ambazo ni lazima zifuatwe. Huwezi kujenga kituo cha polisi kama kujenga duka.

Tuhuma nyingine iliyoibuliwa ni Malisa kuahidi kujenga ofisi na kushindwa kujenga. Kwa kweli hii inadhihirisha mtoa hoja ameamua kupika majungu au labda si mwanafunzi wa SAUT. Ukweli ni kwamba Malisa aliahidi ofisi ili kuwezesha viongozi wake kufanya kazi kwa uhuru zaidi. Lakini hii haimaanishi Malisa hana ofisi. Kwa sasa SAUTSO wana ofisi nne ambazo wanazitumia kufanyia majukumu yao. Japokuwa ofisi hizi ni chache lakini bado serikali ya SAUT ina ofisi nyingi ukilinganisha na vyuo vingine. Kwa mfano UDSM pamoja na kuwa chuo kikongwe lakini bado wana ofisi moja ya DARUSO.

Hivyo suala la ofisi halikuwa sensitive sana japo lipo kwenye ilani ya Malisa. Na ukweli ni kuwa Malisa amepambana hadi ofisi mpya imepatikana. Kwa sasa iko katika hatua za finishing, yani kupiga rangi na kuweka furnitures ndani. Ofisi hii ipo karibu na jingo la Mwanjonde, ina vyumba sita vya ofisi na conference hall ndogo, vyoo na sehemu ya mapokezi. Ofisi hii ikikamilika, itafanya SAUTSO kuwa na jumla ya ofisi kumi. Na hii itamfanya Malisa kuwa Rais pekee wa chuo kikuu Afrika Mashariki na Kati mwenye ofisi nyingi zaidi. Wakati wa mahafali ya chuo November 17 mwaka jana, Malisa alipata fursa ya kumuonesha Waziri wa Ujenzi Mh.John Magufuli ofisi hizo na picha zipo.

Kuhusu Malisa kushindwa kushughulikia matatizo ya mkopo si kweli. Malisa anaweza kuwa Rais anayehangaikia wahanga wa mikopo kuliko waliomtangulia. Ikumbukwe kuwa kama enzi za Rais Fulani hakukuwa na changamoto za mikopo haimaanishi kuwa the said President alikuwa muwajibikaji sana. Kila regime ina changamoto zake. Changamoto za mkopo mwaka huu haziwezi kufanana na za mwaka jana au kinyume chake. Kwa sasa watu wanaomba mkopo kupitia mtandaoni, awali walikuwa wakijaza form ambazo ni hard copy. Sababu hiyo tu ya kubadilisha mfumo tayari inaibua changamoto mpya ambayo haikuwepo awali. Kwa mfano kwa sasa kuna changamoto ya kushindwa ku-update mikopo. Changamoto hii haikuwepo kipindi cha nyuma. Lakini Malisa amefanya juhudi nyingi kutetea watu wake na mara nyingine kwenda mwenyewe bodi ya mikopo. Mafanikio yake yameonekana kwa wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa wamezuiwa fedha zao kwa matatizo ya account number kupata fedha zao mwezi December mwaka jana.

Wanafunzi wengine takribani 250 (si 500 kama inavyodaiwa) serikali inapambana kuhakikisha wanapata fedha zao. Ukweli ni kwamba shida kubwa ipo bodi ya mikopo. Majina ya wanafunzi hao yamewasilishwa bodi yakiainisha matatizo yao na ufuatiliaji wa kina umefanyika lakini bodi kila siku wanakuja na sababu mpya. Lakini bado baadhi ya wahanga walikuwa hawaamini kama kweli majina yao yamepelekwa bodi. Ili kuwafanya waamini Malisa akawaambai wateue watu wawili ambao wataenda Bodi na waziri wa mikopo kufuatilia.

Serikali ya Malisa ikawaombea ruhusa watu hao, Malisa mwenyewe akawapeleka kwa Vice Chancelor  ili kuwatambulisha, na hatimaye Serikali yake ikawagharimia kwa kila kitu tangu usafiri, mawasiliano, chakula na malazi kwa siku zote walizokaa Dar kwenda bodi kuhakiki eti kama kweli majina yao yalitumwa. Hali hii iliiyoonesha ukomavu wa siasa wa hali ya juu alionao Malisa maana ni serikali chache sana zinaweza kuwa na ujasiri kama huu. Hata hivyo watu hao walipofika bodi walihakiki kuwepo majina na maafisa wa Bodi wakawaahidi kuwa fedha yao wataipata January. Hadi hapo hali inaonesha tatizo la mkopo SAUT si Malisa bali Bodi ya mikopo yenyewe.

Katika kuonesha dhana ya uwajibikaji, jumatano ya tar.09/01/2012 Malisa alifanikiwa kuwakutanisha wahanga wa mkopo na Vice Chancelor, ambaye alifanya mawasiliano ya moja kwa moja na Afisa Mtendaji mkuu wa Bodi ya mikopo Bw.Nyatega ambaye aliahidi kuwaagiza watendaji wake washughulikie madai ya SAUT haraka iwezekanavyo. Baada ya hapo Waziri wa mikopo ameendelea kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na maafisa wa bodi na feedback amekuwa akiwapa wahanga wenyewe. Jambo la msingi ni kuwa Nyatega ameahidi fedha zao zitapatikana kabla hawajaanza mitihani mwisho wa mwezi huu. Sasa leo anaibuka mtu na kudai Malisa ameshindwa kuwasaidia kupata mkopo. Ameshindwaje? Tena bila aibu wanahusisha na chama. Hivi CHADEMA ndio imekataa wasipewe hela?

Kwa wanaomfahamu Malisa wanaelewa namna alivyo mwanaharakati. Hachoki wala hakati tamaa kwenye kudai haki. Mwezi July fedha za field zilichelewa na kuleta manung’uniko kwa watu. Malisa na Waziri wake wa mikopo wakaenda kufuatilia Dar, but BOdi ikawajibu hakuna pesa labda hadi August watakapopata hela tena kutoka Hazina. Wangekuwa legelege wangeweza kurudi Mwanza. Lakini kwa kutambua namna watu wao wanavyoteseka waliamua kufuatilia hadi wizara ya elimu. Iliposhindikana wakamtafuta Mbunge wa Nyamagana Mh.Wenje ambaye aliwapigania hadi hela zikapatikana. Katika kuonesha sense of appreciation Wenje akamtaja Malisa kwenye hotuba yake wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya elimu.

 Sasa unaposema Malisa ameshindwa kupigania mikopo, ameshindwaje? Kwanini tunatunga hadithi za uongo ili kupandikiza chuki?? Hata kama umetumwa na chama chako (CCM) je kimekutuma useme uongo? Wewe kuwa mwanaCCM si tatizo, ila tatizo ni hayo unayofanya kwa kivuli cha CCM. Je CCM imekuelekeza hivyo? Kiapo cha mwanachama wa CCM kinasema “nitasema kweli daima, uongo kwangu mwiko” je kupika majungu ndio kweli inayotajwa kwenye kiapo chenu?

Zipo tuhuma za matumizi mabaya ya fedha. Hoja kubwa inayotolewa ni Rais kupanda ndege. Hii haiwezi kuwa sahihi hata kidogo. Ni vema ikaangaliwa essence ya kupanda ndege kabla ya kupika majungu. Kuna wakati taarifa inafika kwa kuchelewa hivyo kunakuwa hakuna alternative zaidi ya kusafiri kwa ndege. Kwa mfano wakati Fulani Rais Kikwete alihitaji kukutana na Marais wa vyuo vikuu Tanzania. Email ikafika ijumaa na kukutana ni jumamosi. Hapo angesafiri kwa bus ili aonekane anabana matumizi?

Lakini pia Safari za nje ya nchi ni ngumu kusafuri kwa basi. Baadhi ya maeneo ya nje ya nchi ambayo amekwenda ni pamoja na Nairobi, Blantire na Lusaka. Je angetumia daladala ili asiambiwe anafuja fedha? Lakini ni muhimu ieleweke kuwa zipo safari binafsi za Mh.Malisa ambazo husariri kwa ndege kwa gharama zake binafsi. So isitafsrike kuwa kila anapopanda ndege ni fedha ya ofisi. Si sahihi, safari nyingine hutumia fedha zake binafsi.

Badala yake Malisa amejitahidi sana kubana matumizi kwa kushirikisha external stakeholders katika baadhi ya matumizi badala ya kutumia hela ya ofisi. Mfano mzuri ni mashindano ya Pro-Life ambayo hufanyika kila mwaka chuoni hapo. Mashindano yale hutumia takribani milioni 7 kuyaendesha. Lakini mwaka huu serikali ya Malisa ilifanya juhudi binafsi na kuwasiliana na kampuni ya Vodacom ambao walifadhili mashindano yote bila kutumia sent yoyote kutoka chuoni. Shukrani za pekee ziwaendee Vodacom Tanzania.

Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Malisa amefanya mengi makubwa SAUT na ametengeneza heshima kubwa sana kwa chama. Ametetea kurudishwa chuoni kwa wanafunzi 16 waliofukuzwa kwa makosa mbalimbali. Kwenye kikao cha Board of Appeals cha tar.21/11/2012 alisimama kidete kuwatetea wenzake na kuwaombea msamaha ambapo wanafunzi wote walisamehewa na kurudishwa chuoni. Mmmoja wapo ni Aliyekuwa mwenyekiti Chama cha wanaosoma Kiswahili. Hivi hata hili hatulioni?

Wanafunzi wa Public Relations mwaka wa tatu, wanafahamu namna alivowapigania na kuwaombea msamaha wasifukuzwe baada ya kufanya fujo kwenye chumba cha mtihani. Badala yake akaomba wapewe onyo la maandishi, na kweli ikawa hivyo. Bado tunasema Malisa hajafanya kitu?

Kama hiyo haitoshi amehakikisha madarasa yote yanafungwa Projector na kurekebisha sound system kama alivyoainisha kwenye manifesto yake na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa hakuna darasa lolote linalosumbua Projector au sound system.
Malisa alipoingia madarakani aliahidi bei ya chakula haitapanda. Bei iliyokuwepo ni tsh.1200 kwa mboga ya nyama n ash.1500 kwa samaki. Na amehakikisha amesimamia hilo na limetekelezeka. Mwezi November mwaka jana baadhi ya Canteen zilipandisha gharama kuwa 1500 kwa 2000. Kwa haraka Malisa akaiagiza wizara ya chakula kuandika barua ya kuwaita wazabuni hao. Lakini kabla ya kikao cha wazabuni, Wizara husika ikaandaka memo na kutoa maagizo ya bei ya chakula kurudi kama zamani wakati taratibu nyingine zikisubiriwa kufuatwa.

Baada ya hapo wazabuni wakaitwa kwenye kikao, mikataba ikapitiwa na bei SAUTSO ikatoa agizo la bei kurudi 1200 kwa 1500 ambayo ndiyo bei elekezi kwenye mkataba. Jamani hata hili hamuoni? Je kama kusoma hujui, je hata picha huoni? Tuache unafiki tuwe realistic. Unaposema Malisa hajafanya lolote wakati kila siku unakula chakula kwa bei ileile ya awali huoni aibu??
Amejitahidi kushawishi management kuboresha miundombinu ya kujifunzia. Kukarabatiwa kwa maabara ya Engineering, kukarabatiwa kwa madarasa na kupigwa rangi ect.

Hivi karibuni Malisa atasaini mkataba na Kampuni ya TIGO Tanzania ambao wamekubali kufanya mradi mkubwa wa kujenga na kukarabati vimbweta vya kujisomea katika maeneo mbalimbali ya chuo. Mradi huo utakaogharimu jumla ya Milioni 57 za Kitanzania, ni juhudi binafsi za Malisa na serikali yake walizofanya na tigo kupitia Mkurugenzi wa tigo kanda ya ziwa Bw.Julius Lymo. Na hii ni katika kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kwani suala la kujenga vimbweta amelitaja kama kipaumbele namba tatu (Refer Malisa Godlisten &Michael Consolatha, SAUTSO Election Manifesto 2012/2013).

Mnamo mwezi wa September 2012, wizara ya off campus ilifanya kikao na wamiliki wa hostels za nje ili kujadili juu ya gharama kubwa wanazotoza kupangisha wanafunzi. Kikao kile kilikuwa na manufaa makubwa maana bei ya hostel za nje ilishuka. Kwa mfano hostel maarufu za MASHA ,zilishuka kutoka Milioni moja na nusu kwa chumba hadi laki tisa. Zipo hostel nyingi zilizoshusha gharama lakini hatuwezi kuzitaja zote hapa. Je hili nalo si lolote? Watu wamefungua vyuo wamekuta bei nafuu, tofauti na waliyoiacha. Wengine hata hawajui juhudi zilizofanyika kupunguza gharama wanaibuka na kudai serikali haijafanya kitu. Jamani muogopeni hata Mungu.

Pia si kweli kuwa Malisa anasafiri sana. Mimi nimekuwa kiongozi kwenye serikali ya Mataba. Kwenye serikali ile Viongozi wanne tu wa juu ndio waliokuwa wanasafiri, Rais, Makamu, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa serikali. Ilikuwa ni ndoto kwa waziri kupata nafasi ya kusafiri. Lakini sasa hadi wabunge wanasafiri, Makatibu wa wizara wanasafiri, Mawaziri hali kadhalika. Safari ya Rwanda Mh.Rais hakusaafiri, aliwakilishwa na Makamu wa Rais. Lakini alitoa fursa kwa baadhi ya mawaziri, naibu mawaziri na wabunge kwenda. Tulikwenda na kukaa siku saba na kurudi.

Safari ya Zanzibar kwenye uchaguzi wa TAHLISO hakwenda licha ya kuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakitajwatajwa sana kugombea. Aliwakilishwa na Makamu wake na viongozi wengine wa serikali.
Jingine ambalo limepotoshwa sana tena kwa makusudi ni michezo ya vyuo vikuu vya SAUT iliyofanyika Morogoro mwezi December mwaka jana. Mtoa hoja anadai heri mashindano ya Mtwara yaliyosimamiwa na Mataba. Akaendelea kupotosha kuwa eti chakula, malazi na usafiri vilikuwa bora kuliko Morogoro. Sasa hebu tutizame facts kidogo mbazo ndizo zitakazoonesha mashindano gani yalikuwa na ahueni kati ya Mtwara na Morogoro.

Mtwara tulienda kwa basi ambalo liliharibika njiani takribani mara nne likitengenezwa kabla ya kufika manispaa ya Mikindani. Hiki ni kiashiria tosha kuwa gari lilikuwa bovu. Morogoro tumekwenda kwa Luxury Bus (YOUTORN) na hatukupata matatizo yoyote njiani. Mtwara tulipewa sh. Elfu 4 na wengine elfu 5 kama gharama ya kujikimu kwa chakula kwa siku. Morogoro tumepewa efu kumi kwa mtu kujikimu kwa siku. Hivi hapo afadhali nani?

Mtwara wachezaji na viongozi wote tulilazwa mabwenini na wengine chuo cha VETA huku Mataba akijitafutia chumba kwenye lodge ya kifahari pale Mikindani. Morogoro Malisa alitangulia kufika so akatutafutia vyumba standard. Wachezaji wote na viongozi tulilala kwenye Lodge nzuri (mojawapo ni Larry Lodge ambayo ni maarufu sana pale Moro). Vyumba vyote vilikuwa ni Self Contained, kila chumba kina TV na kabati. Baadhi ya vyumba vilikuwa na AC na vingine Feni. Hivi bado hatujaona nani bora?

Morogoro mashindano yalirushwa live na TOP Radio, inayosikika mikoa 16 Tanzania bara. Kama haitoshi  Abood Radio, Radio Maria, Planet fm na Clouds fm zilikuwa zikiripoti kila siku. Mtwara mashindano hayakurushwa hata na Radio mbao.

Mtwara tulilala watu wanne kwa chumba, lakini Morogoro tumelala watu wawili kwa chumba. Malisa alijitahidi sana kumotivate timu yake jambo ambalo sikulionaa kwa Mataba Mtwara. Kila goli moja kwa upande wa soka alikuwa analipia elfu kumi. Na kila timu ya Netball waliposhinda aliwapa elfu 20 kama motisha. Hali kadhalika kwa Basket na Volleyball. Fedha hizi hazikuwa za ofisi bali ni fedha binafsi za Malisa. jiulize ni kiasi gani alipoteza kuhamasisha timu yake ya Main Campus. Jiulize siku tulipowafunga Bukoba goli 6 na kila goli alilipia elfu kumi, bado Netball walishinda, Basket nao, Voleeyball pia. Can u count the cost? Kwa kweli hii ni spirit ya ajabu sana ambayo ni viongozi wachache sana wanaweza kuwa nayo.

Kimsingi mashindano yalikwenda vizuri sana isipokuwa wakati wa kutoa zawadi siku ya fainali. Kimsingi ni kwamba tatizo lililojitokeza ni la “technicality” ambalo wala Malisa hakuhusika na engine wala hakuwa anajua. Mzozo ulianza baada ya kamati ya michezo ya mashindano yale kumtangaza mchezaji kutoka RUCO kuwa ni mfungaji bora wakati ana magoli 7, na kumuacha mchezaji wa Jordan aliyekuwa na magoli nane.

Baada ya hapo Jordan wakafunga geti kumzuia Yule mchezaji wa RUCO kwenda kuchukua zawadi, RUCO kuona hivyo nao wakatumia nguvu kumpeleka hightabe mchezaji wao apate zawadi. Baada ya hapo mtafaruku ukuaendele na Jordan wakasusia zawadi zao zote zilizobaki, ikiwa ni pamoja na kombe la ubingwa wa football. Sasa kwenye mazingira hayo unasemaje Malisa kashindwa wakati haikuwa kazi yake kupanga mfungaji bora?

Tuache upotoshaji na tuwe wakweli. Mtu huyu aliyetuhumu anaonekana kabisa anatumiwa na anapotosha kwa maslahi ya watu Fulani. Hii inajidhihirisha maana amemtaja Vice Chancelor (Dr.Kitima)  kuwa ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, wakati Vice Chancelor mwenyewe hakuwepo kabisa kwenye mashindano hayo maana alikuwa nje ya nchi.

Nikiwa kama kiongozi wa serikali ya SAUTSO iliyoko chini ya Malisa naamini Malisa bado ni icon ya SAUT. Amefanya mazuri mengi, mengine tunayaona lakini mengine hatuwezi kuyaona kwa sasa may be hadi aondoke maana waswahili husema thamani ya mtu huonekana pale anapokuwa hayupo.
Kimsingi wanaSAUT bado tuna imani na kamanda Malisa, tunamwamini na tunamheshimu. Ni kiongozi Jasiri, Shupavu na asiye mnafiki. Amekuwa akijitambulisha hadharani kuwa mwanachama wa CHADEMA bila woga wala aibu, tofauti na Marais wengi ambao wamekuwa wanafiki kwa kudai hawana vyama kumbe wanasuport concealed. Waliokuwepo kwenye mahafali wanakumbuka Vice Chancellor alimtambulisha Malisa mbele ya halaiki na mbele ya Mh.Magufuli kuwa Rais wa SAUTSO ni “kamanda wa CHADEMA”

Mwisho nashauri CHADEMA kuwa makini na watu wanaojiita makamanda lakini kazi yao wanapika majungu ndani ya chama. Wengi ni mamluki wanaotumiwa kuharibu image ya chama. Chama hakina makamanda wanaotuhumu bila facts, wanaopika majungu, na kudamage hata image ya chama kwa maslahi binafsi. Huwezi kutoboa Boti uliyopo halafu ukaendelea kujihisi upo salama. Mhe.John Heche aliwahi kusema “hatuwezi kuwa na watu wanaojiita CHADEMA lakini wanafanya kazi za CCM halafu tukawaacha waendelee kubaki ndani ya chama. Haiwezekani” Tuwakemee, tuwapuuze, tuwape onyo ili waelewe kuwa CHADEAMA haina muda wa majungu, ina muda wa kujipanga kuchukua dola mwaka 2015.

Comments

  1. ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha mbona sioni kama waandishi wote wawili elimu mnayoipata hapo saut inawakomboa em kuweni na uhuru wa fikra wote mmeonesha ushabiki kwA marais wenu unaowapelekea kuudanganya uma

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA