SUNGU NA VINEGA WENZIE KUNUKISHA ANTI VIRUS A-TOWN Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ameweka kambi ndani ya A-Town pamoja na Vinega wote, wakifanya harakati za nguvu, kuwahamasisha wananchi wajae kwa wingi Uwanja wa Triple A ambako shoo kali ya Hip Hop itachukua nafasi Desemba 18, 2011 (Jumapili hii). Sugu amesema kuwa yupo kwenye mishemishe kibao, akifanya ‘interview’ kutoka redio moja hadi nyingine za Arusha, kutengeneza uelewa kwa wana wa Arusha kuhusu harakati za Anti Virus zinavyolenga kumkomboa msanii wa Tanzania.Ni Venega wale wale wanaosababisha kizaazaa mtaani kwa mix-tape zao za Anti Virus kisha wakaibua mambo makubwa kwenye Tamasha la Burudani kwa Mashabiki, Muziki unalipa Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam. Taarifa ni kwamba shoo hiyo ya Triple A, itaanza saa 8:00 mchana mpaka saa 6:00 usiku.Sugu ndiye ataongoza shoo hiyo, wakongwe Mabaga Fresh, Big Dog Pose, Hardmad, Zay B na Sister P, wa...