KAFULILA ATIMULIWA NCCR-MAGEUZI

Chama  cha NCCR- Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini,  David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urasi wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura  cha Halmashauri Kuu Nec ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa  Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi. Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”

Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha  kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki , Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa  sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe  hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally  omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.

Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec  kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye cha migogoro yote inayoendelea ndani chama.
“Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu.

Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yeyote inayopenda amani,” alisema Mwasada. chama hicho hivi sasa.Hata hivyo, Kafulila juzi  alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.

“Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu, “ alisema Kafulila na kuongeza:

“Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno  na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam.”

Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.

Aliongeza kuwa, Katibu Mkuu huyo  amefikia hatua ya kutaka  ionekane kuwa wenyeviti wa chama wa majimbo ya mkoa wa Kigoma wanampinga (Kafulila), lakini kati ya wenyeviti  wanane ameambulia wawili tu ambao ndiyo anawanywesha sumu ya chuki dhidi yake.

via gazeti Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA