SUNGU NA VINEGA WENZIE KUNUKISHA ANTI VIRUS A-TOWN
Mbunge
wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ameweka kambi ndani
ya A-Town pamoja na Vinega wote, wakifanya harakati za nguvu,
kuwahamasisha wananchi wajae kwa wingi Uwanja wa Triple A ambako shoo
kali ya Hip Hop itachukua nafasi Desemba 18, 2011 (Jumapili hii).
Sugu amesema kuwa yupo kwenye
mishemishe kibao, akifanya ‘interview’ kutoka redio moja hadi nyingine
za Arusha, kutengeneza uelewa kwa wana wa Arusha kuhusu harakati za Anti
Virus zinavyolenga kumkomboa msanii wa Tanzania.Ni Venega wale wale
wanaosababisha kizaazaa mtaani kwa mix-tape zao za Anti Virus kisha
wakaibua mambo makubwa kwenye Tamasha la Burudani kwa Mashabiki, Muziki
unalipa Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Taarifa ni kwamba shoo hiyo ya
Triple A, itaanza saa 8:00 mchana mpaka saa 6:00 usiku.Sugu ndiye
ataongoza shoo hiyo, wakongwe Mabaga Fresh, Big Dog Pose, Hardmad, Zay B
na Sister P, watafanya kieleweke..
Shujaa wa Kundi la Wagosi wa
Kaya, Fred Mariki ‘Mkoloni’, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’ na mwana Hot Pot
Family mwenzake, Suma G, Mapacha, Dani Msimamo, Rama Dee, Peen Lawyer,
Adili Mkwela ‘Hisabati’, D wa Geto, Magazijuto, Coin Moja, LWP ‘Majitu’
na wengine kibao watakuwepo kuhakikisha wana wa Arusha wanapata burudani
ya ukweli ya Hip Hop.
Mratibu wa shoo hiyo, Mkoloni
alisema kuwa muziki (sound) utakuwa ni wa kiwango cha juu ambao thamani
yake ni shilingi milioni 50.
“Ma-DJ
wenye kiwango cha juu watakuwepo kufanya mambo makubwa. Atakuwepo
mtaalam,Profesa Ludigo. Wasanii watakaokuwepo ni wengi mno,
tutakumbushia mapini ya kitambo na baadaye Vinega watafanya Anti Virus
ieleweke,” alisema Mkoloni.
Comments
Post a Comment