ROBO FAINALI YA MICHUANO YA ProLIFE SAUT: WANAMAHUSIANO YA JAMII WANG’ARA DHIDI YA WAHASIBU; HUKU MECHI YA KWANZA IKISHUHUDIA WANASHERIA WAKISUSIA MCH

Robo fainali ya michuano ya mashindano ya ProLife katika Chuo cha Mtakatifu Agustino, Mwanza imeanza leo pale iliposhuhudiwa michezo miwili ya miamba ya soka chuoni hapo ambapo mechi ya kwanza ilikuwa ni kati ya timu ya Sheria (LLB) dhidi ya Walimu (EDUCATION) ulioanza saa 8 kamili mchana huku mchezo wa pili ulikuwa ni kati ya Mahusiano ya Jamii na Masoko (BAPRM) dhidhi ya Wahasibu (ADA).

Katika mchezo wa kwanza mashabiki waliokuwepo uwanjani walishuhudia mchezo huo ukiishia kati baada ya timu ya Sheria kugomea mchezo huo kutokana na kilichodaiwa kuwa muamuzi wa mchezo huo kufanya maamuzi yalionyeesha dhahiri kuwapendelea timu ya Walimu hivyo mchezo huo kuishia katikati mwa kipindi cha pili na sheria kujitoa katika mashindano hayo hivyo walimu kupita kwenye raundi inayofuata kwa mbeleko hiyo.

Aidha katika mchezo wa pili miamba ya soka ya SAUT timu ya Mahusiano ya Umma ilitoa kipigo cha mbwa mwizi pale ilipowagalagaza Wahasibu kwa jumla ya magoli mawili bila ya majibu katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua ndani ya viwanja vya Raila Odinga chuoni hapo. Kwa matokeo hayo timu ya Walimu na Wanamahusiano zimefuzu katika hatua ya nusu fainali michezo itakayochezwa wiki ijayoKesho tena katika viwanja hivyo vya Raila odinga kutakuwa na mitanange mengine miwili ya robo fainali

Hali ilikuwa si hali pale sheria walipogomea mchezo wao na walimu.

Ilikuwa ni watu kuwa katika vikundi kujadili kilichotokea mara baada ya mchezo huo kuvunjika.

Timu ya sheria ikikusanya jezi zake baada ya kugomea mchezo huo.

Kikosi kizima cha timu ya Mahusiano ya Jamii na Masoko.

Kikosi kamili cha Timu ya Wahasibu ((ADA).

Vikosi vyote vikipata nasaa toka kwa Fr. Maziku kabla ya kuanza mchezo huo.

Wachezaji wa Timu ya Mahusiano ya jamii wakishangilia goli la pili.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA