KUTOKA SAUT:COLLAGE BARAZA YAFANYIKA
Kutoka
chuo kikuu cha Mt.Augustine,leo imefanyika collage baraza ambapo imewakutanisha
Makamu mkuu wa chuo (VC Charles Kitima), Dean Of Students (mama Nasania),
Corporate counsel, serikali ya wanafunzi (SAUTSO) pamoja na wanafunzi wa chuo
cha SAUT kwa pamoja kwa ajili ya kuzungumzia kero mbalimbali ambazo
zinawakabili wanafunzi wawapo ndani na nje ya chuo,mengi yamesemwa na wanafunzi
na kutolewa ufafanuzi na Makamu mkuu wa chuo.
Yafuatayo
ndio yaliweza kutolewa ufafafanuzi na makamu mkuu wa chuo.
1. Swala la ulinzi hafifu ndani na nje ya chuo,Makamu mkuu wa chuo ametoa
ufafanuzi kuwa swala hilo limeshafika chini ya uongozi wake na wanalifanyia
kazi hasa kwa kuboresha kampuni ya ulinzi iliyopo chuoni kwa kuongeza idadi ya
walinzi wengi wa kufanya patrol kila wakati,pia swala la kujenga kituo cha
polisi eneo la Nsumba amesema kuwa “Hakuna haja ya kujenga kituo cha polisi
Nsumba kwa sababu polisi wanawekewa lita za mafuta kwenye gari zao kwa ajili ya
kufanya patrol eneo lote la chuo hivyo hata kikijengwa bado itawabidi wafanye
patrol tu eneo zima hivyo kituo kilichopo Nyegezi kinatosha.”
2. Ulipaji wa faini ya shilingi laki moja, VC Kitima amesema kuwa wale
wote wanaochelewesha ulipaji wa ada bila sababu za msingi basi lazima faini hiyo Wailipe ametoa msimamo wake
kwa kusema kuwa “hatakuwa na msamaha
kabisa kuhusu faini hiyo”,akaendelea kutoa ufafanuzi kuwa kwa wanafunzi ambao watakuwa
na matatizo yoyote kuhusu ada basi wafike katika ofsi ya DVCAF - father
Mwanjonde kwani ndiye amepewa mamlaka yote yanayohusiana na swala la ada na
mambo mengine yote yanayohusiana na fedha.
3. Tatizo la lugha chafu inayotolewa na baadhi ya wafanyakazi wa chuo,VC Kitima amesema swala hilo
atalifuatilia kwa ukaribu kabisa na kwa wote watakaobainika kufanya hivyo basi
hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kusimamishwa kazi,wanafunzi wamekuwa
wakilalamikia baadhi ya ofsi za chuo ambapo wamekuwa wakikutana na lugha
zizizolizisha na saa zingine kuambulia matusi,na ofsi hizo zilianikwa wazi kuwa
ni kwa mkuu wa idara ya Elimu (Mabere),ofsi wa wahasibu wa chuo, ofsi
inayohusika na mikopo ya wanafunzi.
4. Tatizo la miundo mbinu kwa wanafunzi wenye ulemavu, chuo kimeonekana kutokuwa na
miundombinu ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kupanda ngazi wakati wa
vipindi au Makitaba kwenye magorofa makamu katolea ufafanuzi kuwa majengo yote
hayo yanasehemu maalum kabisa kwa ajili ya kuweka lift zitakazo ondoa tatizo
hilo lakini bado imeshindikana kwa sasa kwa sababu ya tatizo la uchumi ambalo
linaikabili nchi na hata chuo chenyewe akaendelea ksema kuwa gharama ya kununua
lift moja ni sawa na kujenga darasa moja kama M13.
5. Uwepo wa kozi nyingi kwa muhula mmoja, wanafunzi wamekuwa
wakilalamika sana juu ya kuwepo masomo mengi mpaka kufikia kozi 12 kwa semester,VC
Kitima kasema kuwa hii ni private university ina sheria zake za kiutendaji
hivyo kozi hizo haziwezi kutolewa na nia siyo kumuumiza mwanafunzi bali ni
kumweka katika mazingira mazuri ya kupata maarifa ya kutosha ili aweze kuendana
na soko la ajira na kuweza kumweka mwanafunzi wa SAUT kuwa tofauti na wanafunzi
wa vyuo vingine.
6. Tatizo la mikopo ya wanafunzi, wanafunzi wamekuwa wakilalamika juu ya ucheleweshwaji
wa mikopo yao na wengine majina yao kutokutolewa kwa wakati,Makamu mkuu kasema
kuwa swala la mikopo ni mkataba kati ya bodi na mwanafunzi husika na sio SAUT
lakini wao wanaweza kusaidia pindi
panapobidi,akafafanua kuwa mpaka sasa hivi bodi bado hawajotoa fedha za ada kwa
wanafunzi wanaonufaika na mikopo hiyo,hivyo kuna uwezekano wanafunzi wasifanye mitihani
ya mwisho wa semester ya kwanza.
7. Tatizo la uhaba wa computer makitaba na internet, VC Fr. Kitima ameweka bayana
kuwa swala hilo linafatiliwa kwa ukaribu kabisa na tayari wamefunga mkonge wa
Taifa wa Internet na hivi punde utaanza kutumika hapa chuoni na pia kawapa
ushauri wanafunzi wajitahidi wanunue laptop ili waweze kwendana na mabadiliko
ya sayansi na technolojia.
Mambo mengi yamezungumzwa pia mafanikio yamewekwa
bayana mfano chuo kimeweza kuajiri wahadhili mbalimbali kutoka sehemu
mbalimbali za dunia kwa nia moja tu ya kuweza kuimarisha na kutoa elimu
bora,pia mkuu kasema yuko tayari kuajiri mhadhili yoyote kwa bei yoyote ili
kuweza kuboresha elimu.VC kapongeza pia serikali ya wanafunzi kwa kuwajibika
vizuri na pia kushirikiana na uongozi wa chuo, Makamu pia katoa nasaha zake kwa
wanafunzi wote hasa wasichana kujiepusha na kwenda night clubs kwani hazina
umuhimu wowote bali zinaharibu performance katika taaluma.
Comments
Post a Comment