Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez mara baada ya kuwasili Shule ya Msingi ya Kawawa iliyopo Manispaa ya Kinondoni kupokea msaada wa madawati 500 kutoka Kampuni ya Simu ya Tigo Dar es Salaam leo asubuhi. RC Makonda akisalimiana na wafanyakazi wa Tigo. Ofisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea madawati hayo. Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupokea msaada huo. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza katika mkutano huo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza katika hafla hiyo wakati akipokea msaada huo. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kawawa wakipiga makofi wakati wa kupokea msaada huo. Wanahabari nao walikuwepo kuchukua taarifa h...