ZOEZI LA UCHANGUZI LINAENDELEA VISIWANI ZANZIBAR

Wananchi wakipiga kura katika kituo cha Skuli ya Muembeladu

Baadhi ya wananchi wakihakiki majina yao kabla ya kuingia kupiga kura katika kituo cha skuli ya Raha Leo.


Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza.

katika baadhi ya vituo nilivyopata kutembelea asubuhi hii wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa.

katika kituo cha shule yasekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita na vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91 akizungumza msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe .

kwa upande wa kituo cha skul ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu kupiga kura, zoezi hilo limeanza vizuri kwa katika eneo hilo la Muembe shauri ambapo ni Jimbo la Raha Leo.

Zoezi katika Jimbo la kikwajuni linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa waliojitokeza kupiga kura ambapo katika kituo cha skul ya Raha Leo.

Wakizungumza baadhi ya wananchi walijitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua rahisi na amani tofauti na taarifa zilivyokua zinsambazwa katika mitandao.

Mkazi wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga kura linaendelea kwa amani na utulivu.

Aidha ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kusimama imara na wa moja katika kipindiki ambapo watu wasio takia mema Zanzibar wakijitahidi kutaka kuwagawa wazanzibar kwa misingi ya ikikadi za kisiasa.

“ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu ambao wahaitakii mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu”amesema Haji
Wakati zoezi hilo linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanya biashara wakiendelea na kazi kama kawaida,kwa upande wake mfanyabiashara Musa Jackson amesema zoezi limekua safi na kuomba wananchi wajitokeze.

Amesema kuwa ni vyema watu wajitokeze kuchangua viongozi na kuacha kususia uchanguzi huo,”wananchi wajitokeze waache kususa kwani haisadii na kufanya hivyo ni kupoteza haki yako”amesema

katika jimbo la Mpandae zoezi linakwenda vizuri kwa wakinamama wengi kujitokeza katika skul ya Jangombe.

Chanzo: http://kamerayangu.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA