JWTZ WATOA TAARIFA KUHUSU UVUMI ULIOENEA MITANDAONI

jwtz 2
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016.
Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu.
Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.
JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.
CHANZO:MJENGWABLOG

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA