Shy-Rose Bhanji Amwonya Msekwa
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shy-Rose Bhanji, amemshutumu Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na kumtaka aache kukifanya chama hicho kama mali yake. Shy-Rose ambaye aliwania ubunge katika Jimbo Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kushindwa kwenye kura za maoni, alitoa kauli hiyo jana akijibu kauli ya Msekwa ya juzi akiwataka wanaotaka kuhama chama hicho baada ya kushindwa kwenye uteuzi wahame haraka. Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Shy-Rose alisema ameshtushwa na kauli ya Msekwa kwani hakuwa na haki ya kutamka maneno mazito na yasiyo ya kiungwana hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. “Kwa kweli nilivyosoma gazeti moja leo nimekutana na habari hii, ikanishtua kidogo. Nikajiuliza hivi huyu mzee Msekwa anasema maneno ya ajabu namna hii, hiki chama ni chake binfasi? Pengine amejisahau kwamba CCM ni chama chetu wote, sasa iweje yeye awe na ujasiri wa kujiamini kutoa maneo ya ajabu wakati hiki ni chama chetu wote au yeye anadhani ni chama