PROFESA JAY KUPAGAWISHA DALLAS LEO JUMAMOSI


PROFESA JAY

The heavy weight Mc, Profesa Jay Jumamosi hii anatarajia kupanda katika jukwaa la Murphy's Place Dallas nchini Marekani, baada ya 255 kumsaka Profesa Jay kwa muda mrefu bila mafanikio hatimaye leo majira ya saa sita za mchana mtu mzima akavuta wire,jamaa tayari ameshapiga show Houston Texas, Washington DC, Boston na sasa hivi yupo mjini Dallas na akiendelea na maandalizi ya Show ya Jumamosi.

Aidha Prof alielezea ziara yake aliyoifanya mwezi uliopita katika makao makuu ya taasisi ya Malaria no More yaliyopo jijijini New York, prof anasema yeye kama balozi wa malaria aliweza kukutana na jopo la zima la Taasisi hiyo, na alifanya vitu vingi ambavyo alishindwa kuvitaja vyote, Prof alitumia fursa hiyo kuziasa jamii zote zinazo athirika na ugonjwa wa malaria, kwa kusema kila mtu apigane kwa uwezo wake ili kuutokomeza ugonjwa huo unao ongoza kwa kuua watu wengi nchini.

Profesa alimalizia kwa kusema "Malaria haikubaliki" ukitaka kufahamu mengi tuliyozungumza na Profesa Jay pamoja na CEO wa Kampuni inayosimamia Tour za Profesa Jay nchini Marekani.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA