Ufunzi wa Hasheem Thabeet kwa vijana waanza



Mchezaji wa ligi kuu ya mpira wa Kikapu nchini Marekani, almaarufu, NBA, akiichezea timu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet yupo nyumbani Tanzania kwa lengo la kuwafunza vijana mbinu sahihi za mchezo huo kupitia programu maalumu ya Basketball Clinic .

Jana katika ukumbi wa ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Hasheem alizungumza na waandishi wa habari akielezea kuwa programu hiyo rasmi jana tarehe 12 Agosti 2010 kwenye viwanja vya Don Bosco.


Watoto zaidi ya 400 wanatarajiwa kukutana kwenye clinic hiyo. Makamu Mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa kikapu nchini, Tanzania Basketball Fedreration (TBF) bw. Phares Magesa amewataka vijana wote watakaotaka kushiriki mafunzo haya kujiandikisha katika shule zao zenye vilabu vya mchezo wa basketiboli.

Hasheem alisema kuwa programu hii imeshaendeshwa katika nchi kadhaa barani Afrika zikiwemo Nigeria, Senegal, Ivory Coast na sasa Tanzania. Barani Asia alishirikiana na Yao Ming kuendesha programu iyo hiyo kwenywe nchi za HongKong, Quatar na Taipei

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA