ALICHOKISEMA FID Q TZ HipHop!
Fid Q. Miaka 11 ya “FidQ.com” Kitu chochote kile kinaweza kuchukuliwa kama kazi ya sanaa, ila inategemea mtazamo wa hadhira ukoje juu ya kitu au kazi husika. Kwa upande mwingine, historia — hasa za jamii au vikundi vya jamii vilivyokuwa na vinavyoendelea kukandamizwa kwa namna moja au nyingine — husema vingine. Sanaa imekuwa ni mojawapo ya zana zinazotumiwa kufungua macho na fikra za watu kwenye jamii mbalimbali, katika vipindi tofauti. Mfano mzuri ni ndugu zetu wa Afrika Kusini. Wakati wa utawala wa kibaguzi (herufi ndogo zimetumiwa kwa makusudi), watu waliokuwa wanaangaliwa kama viongozi walikuwa hawaruhusiwi kukutana au kuongea na mtu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Lakini harakati zao hazikugota; waligeukia sanaa — wakatumia kazi za sanaa kuamsha watu. Kwa hapa nyumbani, historia sio tofauti sana. Wazazi wetu waliokuwa kwenye harakati za kuusaka Uhuru walitumia mpaka ngonjera za mashuleni kuwasilisha sera za TANU, ASP na vyama vingine vya siasa. Kiz