DALADALA IN ROCK CITY.....

Daladala katika mitaa ya Mwanza.
Kile kipindi cha Daladala kinachorushwa kila siku kupitia ITV kikifanyika ndani ya Daladala ambamo humo abiria hujadiliana masuala mbalimbali yanayozunguka katika harakati za maisha yao ya kila siku, sasa ni zamu ya mkoa wa Mwanza hivyo basi ukikutana na Daladala maeneo ya Nyegezi, Kilimahewa, Pansiasi, Igombe, Igoma, Mabatini, Magu na kwingineko kote panda kisha husika....

Mtangazaji wa kipindi cha Daladala kinachorushwa kupitia ITV Daniel Kijo akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Erenest Ndikilo, pindi crew ya kipindi hicho ilipodhuru ofisini kwa mkuu huyo jijini Mwanza leo tayari kuanza shughuli zake rasmi kuanzia wiki ijayo siku ya jumatatu.

Jenerali Ulimwengu akizungumzia mdahalo wa Uhuru wa vyombo vya habari uliofanyika jana katika chuo cha SAUT -Mwanza
.
Mdahalo ulilenga kuainisha maeneo yanayohusiana na uhuru wa vyombo vya habari ni changamoto zipi, matatizo yapi, wapi kunahatarisha uhuru wa tasnia ya habari, ni namna gani ya kuikwepa hali hiyo na kila mtu anamajukumu yake iwe ni Mwandishi wa habari, wahariri wao, wamiliki wa vyombo vya habari, jamii kwa ujumla vyama vya siasa, serikali na nk kila mtu majukumu yake yameainishwa yote ni kwaajili ya kuboresha maisha yao kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Umma uliohudhuria mdahalo uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu Cha Sauti jijini Mwanza.

Sahihi kwa kitabu cha mada kilichozinduliwa.

Mwanafunzi kutoka SAUT akizungumza na kipindi cha Daladala.

Nashukuru sana vijana wenzangu kuonyesha uvumilivu wa hali ya juu katika mdahalo wa leo kwani katika mijadala mingi ya miaka ya sasa tumezoea kuona watu wakizomeana, kukatishana kabla mtu hajamaliza kuzungumza na mambo kama hayo...

Joseph mwanafunzi wa SAUT akitoa maoni yake


Kijana ukimpa nafasi na siyo kumwezesha tu, atasema kitu na hiyo nafasi itatumika na ninandoto kuwa siku moja uhuru wa vyombo vya utakuwepo kwani serikali itakuwa ikitenda kazi kwa wananchi na siyo serikari iliyo bosi kwa wananchi. 
habari na picha ni kutoka  blog ya   www.gsengo.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA