|
Manusha Sarawan akielezea mchakato ulivyokuwa hadi kumpata Rose Muhando |
Mtumishi
wa Mungu na muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Dodoma Tanzania Rose
Muhando ametangazwa kuwa msanii wa kwanza Afrika kuchaguliwa kuingia
mkataba na kampuni kubwa na maarufu duniani inayojihusisha na biashara
ya muziki ya SONY ukiachilia mbali wasanii kutoka nchini Afrika
Kusini.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Sonny Mama Manusha
Sarawan, Mchakato huo ulishirikisha zaidi ya wanamuziki 100 kutoka
barani Afrika na Rose akaibuka mshindi.Mkutano wa kumtangaza Rose mhando
kama mshindi wa shindano hilo ulifanyika leo katika Hoteli ya
kilimanjaro.
|
Bahati Bukuku, Diamond pamoja na Ali Kiba wakifuatilia kwa makini mkutano huo hivi leo |
kampuni
za Sony na Rockstar 4000 iliyowahi kumpa msanii wa bongo fleva Ally
Kiba jukumu la kufanya nyimbo ya pamoja na R.kelly ndio zimetangaza
kuhusu jambo hili leo Dar es salaam.Mwakilishi wa Rockstar 4000 upande
wa kipaji Afrika Seven Mosha amesema japo kwa sasa hawawezi kutaja
kiwango cha pesa atakachopata Rose Muhando baada ya kupata hilo dili,
mkataba wake ni wa miaka mitano.
Amesema
baada ya movie zake kutengenezwa, vitabu vyake pamoja na vitega uchumi
vingine ndio wataanza kutaja mapato yake.Seven amesema katika mchujo
walioufanya mpaka kumpata Rose Muhando, ulihusisha wasanii wengine nane wakubwa wa Tanzania, waimbaji wa Gospel na Bongo Fleva na pia walikua na idadi nyingine kubwa ya wasanii wa nchi nyingine za Afrika kama Nigeria ambapo mwishoni mtumishi wa Mungu Rose Muhando akashika nafasi ya kwanza.
|
Wanamuziki wa injili John Shabaani na Bahati Bukuku wakimpongeza Rose Muhando ukumbini hapo. |
Katika
mkataba huo, tayari Rose Muhando amerekodi album nzima Afrika kusini
kazi ikiwa imesimamiwa na Sony ambapo amepata nafasi ya kushirikiana
katika nyimbo na na wanamuziki wengine wakali wa gospel wa nchi hiyo
ambao watatajwa hivi karibuni.
Rose
Muhando amekuwa akifanya vizuri kwenye Mauzo ya album zake na kwa sasa
ndiye Mwanamuziki anayeongoza kwa mauzo ya album zake nchini. Kwa mujibu
wa Seven amesema mkataba huo haumfungi Rose Muhando kurekodi nyimbo
zake na studio yoyote Tanzania, japo mpango wa Sony sasa hivi ni
kumpeleka juu zaidi kwenye mauzo ya kimuziki Afrika ambapo atatumia
lugha hiyo hiyo ya kiswahili.
|
Rose Muhando ameingia katika orodha ya wanamuziki mbalimbali wakubwa Duniani wanaofanya kazi na Kampuni ya Sonny. Music |
Comments
Post a Comment