Posts

KUMBE ABIRIA NAO WANAPENDA NJIA ZA SHORTCUT

Juzi nilikuwa natoka Shinyanga katika miangaiko ya hapa na pale,nilikuwa nimepanda basi la AM linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Tabora na Mwanza,mimi nilipandia shinyanga kurudi Mwanza,sasa kilichonishangaza ni kwamba serikali inajitahidi kuboresha barabara zetu ili magari yaweze kupita katika barabara za lami lakini bado kuna madereva wengine hawazitumii barabara hizo na kufanya wao wanavyojua. Tulipita katika barabara ya (Old Shinyanga Road) barabara ambayo haina lami lakini pia kuna vumbi sana kiasi kwamba mwili wote ulikuwa umeogeshwa kwa vumbi la barabara hiyo,nilijaribu kuwadadisi abiria wenzangu hivi ni kwa nini dereva hatumii barabara ya lami anapita huku kwenye barabara isiyokuwa na kiwango walinijibu kuwa "Njia hii ni shortcut kuliko tukitumia barabara ya lami" nikajaribu kujiuliza maswali hivi hata abiria wao wenyewe wanapenda mambo ya shotcut na wako satisfied kabisa na jambo hili,kama mdau wa bolg hii mawazo yako ni yapi kuhusiano na jambo hili??????

17 MARA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA MOROGORO

Na Shomari Binda, Timu ya soka ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Mkoa wa Mara leo imeahidi kuitoka timu ya vijana ya Mkoa wa Morogoro katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali kwenye uwanja wa karume jijini Dar es salam. Akizungumza kwa njia ya simu na BINDA NEWS kutoka jijini humo,Meneja wa vijana wa Mara Sindbad Madenge amesema kikosi cha vijana wake wapo katika hali nzuri katika kuingia katika mchezo huo na kudai kuwa kikosi chao hakina majeruhi yeyote na wapo tayari kwa mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni. Alisema kuwa kitendo cha kuwaondosha katika michuano hiyo mabingwa watetezi timu ya mkoa wa Kigoma kimewaongzea hali wachezaji wake lakini amewataka kutobweteka na matokeo ya mchezo huo katika hatua ya 16 bora. Katika hatua nyingine Madenge ametuma salama za rambirambi kufuatia kifo cha mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoani Mara Fabian Samo kilichotokea Julai 10 na kuiomba familia yake pamoja na wadau wote wa michezo Mkoa

POLENI KWA USUMBUFU

Poleni sana kwa usumbufu uliojitokeza kwa kipindi chote kwa wale wapenzi wa blog hii ,nilikuwa katika kipindi cha mitihani hivyo nilikuwa sipati kabisa muda wa kutosha kuweza ku uptodate information za kutosha,lakini hivi sasa msijali tena nimesharudi so more information zitakuwepo za kutosha.Pia nawashukuru sana na sana kwa kuweza kunipigia kura za kutosha mpaka kuweza kuibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha blog bora za kitanzania kwangu ni heshima kubwa sana lakini pia ni heshima kwa wapenzi wote wa blog hii kwa kuwa wamefanya chaguo halisi. Nawatakia kazi njema za kulijenga Taifa.

THE WINNER......

Image

OMMY DIMPOZ NA DJ ALLY WASHIRIKI PARTY YA KUZINDUA STONE CLUB MPYaaaaaaaa.

Image
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz usiku wa kuamkia leo (nikimaanisha jana alhamisi) ameshiriki vyema kwenye party ya kuzindua Stone Club ambayo imekuja kivingine, na sevis mpya na wahudumu wapya  mara baada ya ukarabati wa muda mrefu.  Party hiyo iliyokuwa ya kimya kimya ilinogeshwa na dance la nguvu lililomwagwa na Ommy Dimpoz akishirikiana na densaz wake mahiri. Dance likiendelea katika stage ndani ya party hilo ambapo usiku huo pia ulitumika kama usiku wa kwanza mara baada ya wanavyuo kumaliza pepa. On the one and Two alisimama Dj Ally ' mzee wa kitu juu ya kitu' toka A- town ambaye alifanya makamuzi ya hatari uspime ndani ya Stone Club Mpyaaa iliyofungwa sound full kiwango ..... Dj Ally amesaini 'kontrakti'  ya muda wa kutosha hivyo ataendelea kukisanukisha hapa. Ommy Dimpoz kwa poz akicheza na shabiki wake mara baada ya mzuka kumpanda...

VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO J3

Image
. . . . . . . . . . . . . .

FAINALI EURO 2012 , SPAIN 4 – ITALY 0

Image
Fernando Torres, Juan Mata, Silva na Alba ndio wameandika hizo nne za Hispania. . . . . .

WAZIRI MKUU AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA KITAIFA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Image
 Wazi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikabidhi zawadi ya cheti mshindi wa kwanza wa jiji lililofanya vizuri kwenye maonyesho hayo kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.  Waziri mkuu mh. Pinda akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ndikilo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho hayo toka halmashauri mbalimbali nchini zilizoshiriki.  Watumishi wa ofisi ya TAMISEMI wakiwa kwenye banda la maonyesho la ofisi hiyo katika viwanja vya CCM Kirumba wakisubiri kutoa maelezo kwa waziri mkuu ambaye alipita kutembelea mabanda ya maonyesho.  Picha ya mchoro wa Jengola kisasa la kliniki ya wajawazito na watoto lililokwisha anza ujenzi wake katika eneo la mtaa wa Utemini jijini Mwanza ambalo likikamilika ujenzi wake litakuwa na taswira hii. Jengo hili litakuwa mbadala wa jengo ambalo linatarajiwa kuvunjwa la Kliniki ya zamani  lililopo mtaa wa barabara ya Makongoro. kupisha ujenzi wa jengo la Benki kuu ya Ta

ASANTENI WADAU KWA KUNIPA USHINDI

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo linatokea katika maisha yangu kila kukicha,pia na kuwashukuru Ndugu,jamaa na marafiki walioko katika mtandao wa facebook kwa kuweza kunipigia kura za kutosha na kuweza kufanikisha kuibuka mshindi katika shindano la kutafuta blog bora za kitanzania ambalo limefanyika zaidi ya miezi 2 katika kupata washindi. Shindano hili linaratibiwa na website ya www.tanzanianblogawards.com ambayo ilianzishwa mwaka jana na mwaka huu shindano  limefanyika kwa mara ya pili likiwa na nia ya kuweza kutangaza blogs mbalimbali ambazo zinamilikiwa na watanzania waliopo nchini na wale waishio ng'ambo lakini pia kuweza kuwathamini kwa kile wanachokifanya katika kuhabarisha jamii kwaa ujumla. Shindano ili lilianza miezi 2 iliyopita kwanza kwa kuweza kunominate blog ambayo inafaa kuingia katika category mbalimbali ambazo zilikuwa zimeanishwa na waratibu,kwa mwaka huu zaidi ya blog 600 za kitanzania zilipendekezwa kuingia katika shindano hili na

BBM PARTY 2012 @Mbalamwezi Beach

Image

WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA POLISI HADHARANI

Na Thomas Dominick Musoma JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limetoa majina ya vijana ambao wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya usaili wa kujiunga na jeshi hilo ambapo kanda ya ziwa utafanyika Julai 2 hadi 4 mwaka huu katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza. Akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma alisema kuwa majina hayo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo katika ofisi za Mkoa na wilaya zote. “Mwaka huu tumeamua kuchukua vijana watakaojiunga na jeshi letu kutoka mashuleni ambao wamemaliza kidato cha nne mwaka jana na cha sita mwaka huu hivyo tunawaamba vijana wote waende wasome na wajue kama jina lake lipo katika orodha yetu,” “Hii tumerahisisha ili kupunguza msongamano wa vijana kufika katika ofisi zetu na kuulizia ajira hizo na kama unatumia mtandao tafuta katika mtandao wetu wa www.policeforce.go.tz na utaona jina lako na vituo vya usaili,”alisema. Alisema kuwa vijana ambao

TANESCO YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA

 SHIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu. Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao. “Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra. Alisema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo. “Tutatoa namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema.