GHARAMA ZA MATIBABU VYUONI NI MRADI WA VYUO HUSIKA?
MAKALA HII IMEANDALIWA NA ANTHONIUS CLEMENT Mwanafunzi wa chuo kikuu cha mt.Augustino anayesomea shahada ya mahusiano ya Umma na Masoko mwaka wa pili. Email: tonyboy1989@yahoo.com Mobile: + 255 717437729 /+255762 963674 Wengi wetu tunafahamu juu ya umuhimu wa Afya katika jamii yoyote ile. Jamii yenye Afya bora ndiyo yenye maendeleo makubwa kijamii na hata kiuchumi. Nakatika suala hili siwezi kusita kumzungumzia mwanazuoni anayea julikana kama Vans Parkard mwanazuoni huyu wa saikolojia na masomo ya sayansi ya jamii na hasa mawasiliano aliweza kuanisha mahitaji makuu nane ya mwanadamu, Moja ya hitaji hilo ni hitaji la kuishi muda murefu (Imotarity needs) . Hitaji hili ndilo linalo wafanya watu wahangaike kwa muda mrefu waki jipodoa ilimradi tu waonekane bado vijana wabichi. Mwaka mmoja nanusu uliopita Watanzania tuliweza kushuhudia wananchi wengi wakifurika katika kitongoji cha Semunge huko Loliondo alimaarufu “ kwenye kikombe cha babu” hii inadhirisha um