CONDOM KUONGEZWA AFRIKA KUSINI


Maafisa wa kamati inayoandaa michuano ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini, wamesema mipira ya Condom itasambazwa kwa wingi wakati wa dimba hilo.
Maafisa hao wanasema hatua hiyo inanuiwa kuzuia maambukizi ya ukimwi wakati huo.

Daktari anayesimamia maswala ya afya katika kamati hiyo, Victor Ramathesele, amesema wingi wa watu watakaozuru afrika kusini, na hali ya sherehe itakayokuwako imewalazimu kuweka mikakati ya kipekee ya kuwakinga watu.

Afrika kusini ni moja ya mataifa yenye idadi kubwa zaidi ya watu wenye virusi vya ukimwi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA