Siri ya mtungi aijuaye kata- King Kibaden

Habari zilizonifikia hivi punde zinaeleza kuwa Klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Manyema Rangers maarufu kama mkuki wa sumu, imemtimua kazi kocha wake mkuu mwenye machachari Abdallah King Kibaden.

Chanzo cha habari kinaeleza kuwa sababu halisi ya kumwachisha kazi kocha huyo ni kutofanya vizuri kwa Manyema, baada ya kufungwa mechi nyingi za ligi kuu mfululizo na kutishwa na mstari wa kushuka daraja.

Kwa mujibu wa Kocha huyo mwenyewe maarufu kama King Kibaden, repoti hiyo ya Klabu imempa ahueni kwani anajisikia kutua mzigo mkubwa kichwani mwake.

รข€˜kulikuwa na matatizo mengi, na wanasema siri ya mtungi aijuaye kata amesema Kibaden huku akieleza kuwa yeye ndiye anayejua kilichokuwepo ndani ya Klabu na kwamba kulikuwa na mchanganyiko wa mambo mengi yaliyoleta ugumu katika mafanikio.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA