AFANDE SELE ATOA SOMO KWA WASANII WA BONGOFLEVA



Muhimu ni kwa artist wa Bongofleva wenye majina kuwa tayari kukutana wote katika mikutano inayoendelea sasa ikiongozwa vyema na wasanii wenzetu ambao wameshalipia ada ya chama chetu BASATA na tayari mikutano inaendelea mara kwa mara japo mara nyingi wanaojitokeza ni artist wenzetu wakubwa kwa wadogo lakini si wale wanaoaminika kuwa na majina makubwa. Watambue kwamba wakati ndio huu wa sisi kutambulika kama wasanii ili tuweze kudai na kupata haki zetu tunazostahili toka katika vyanzo kibao vya michongo vilivyopo kwa ajili ya muziki wetu, vitu kama usambazaji, udhamini na mambo kibao ambayo leo yanakuja lakini wanachukua watu ambao kimsingi ndio wanaotutesa na kutunyima dili miaka yote. Rais alisema tumueleze shida zetu, wajanja wakasema eti shida yetu ni studio tu, wakati tuna matatizo kibao ya msingi ikiwemo sheria ya haki miliki katika katiba ilivyopitwa na wakati na mambo kibao yanayosabisha artist wakila bia mbili,tatu wanafulia!.

Ila artist wa kibongo hasa wale wanaojitambua lazima wabadilike sasa, wajifunze toka kwa wasanii wa maigizo(filamu za bongo)ambao wameanza kueleweka na kuingiza kazi sokoni juzi tu lakini tayari wana umoja wenye nguvu na chama chenye uongozi kiasi kwamba hata wanapoitwa na viongozi wa serekali wanapata mwaliko kupitia chama chao na wanakwenda wasanii wote wenye akili na wanaoeleweka ili kueleza matatizo yao ya kweli

Watu wanatakiwa wajue kwamba Woga Wetu Ndio Umasikini Wetu, kaburi chakavu la shujaa ni bora kuliko nyumba angavu ya mtu muoga na mnafki

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA